MWANAMUZIKI wa Hip Hop anayefanya poa kwa sasa hapa Bongo, Shariff Thabeet ‘Darassa’, leo amefanikiwa kuisimamisha Ilala alipokutana na mashabiki wake kabla ya Jumamosi hii hajapanda kwenye Jukwaa la Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.
Darassa na Roma, kwa pamoja watapanda katika Jukwaa la Dar Live kwenye Mkesha wa Mwaka Mpya ili kumaliza ubishi wa nani mkali wa michano katika pambano la Nichane Nikuchane.
Akiwa kwenye Viwanja vya Karume jijini Dar, leo, Darassa aliisimamisha
Ilala pale alipotoa burudani fupi ikiwa ni kionjo kabla ya shoo yenyewe
kamili ya siku hiyo.
Akizungumza na mashabiki wake, Darassa alisema: “Mashabiki zangu, siku hiyo ya Mkesha wa Mwaka Mpya mnachotakiwa kufanya ni kuja kwa wingi pale Dar Live kushuhudia miujiza nitakayoifanya kwani siku zote naamini huwa nafanya miujiza kila ninapopanda jukwaani.”
Naye Meneja wa Global Publishers ambao ni waandaaji wa pambano hilo, Abdallah Mrisho, alisema: “Shoo hii inayoenda kufanyika ni ya tofauti, kama tujuavyo R.O.M.A na Darassa kwa sasa ndiyo habari ya mjini hasa kwenye Muziki wa Hip Hop, hii ni mara ya kwanza kwa Darassa kupanda kwenye Jukwaa la Dar Live, hivyo mashabiki ni fursa yenu kujumuika naye siku hiyo.”
Meneja wa Dar Live na mratibu wa mpambano huo, Juma Mbizo akitoa maelezo kuhusu shoo hiyo kwa wanahabari.
Katika hatua nyingine, Meneja wa Dar Live na mratibu wa mpambano huo, Juma Mbizo, alisema: “Kwa kiingilio cha Sh 5,000, mashabiki watapata fursa ya kuingia na kushuhudia mpambano huo mkali ambao rasmi utaanza saa 7 mchana mpaka majogoo.”
Mashabiki wakisukuma gari la Darassa.
Mbali na wakali hao kupanda jukwaani siku hiyo, pia wengine watakaotoa burudani ni pamoja na Kundi la Muziki wa Taarab la Jahazi, Juma Nature, Makhirikhiri, MC Darada, Topido, ID Classic, H-Mbizo na wengine wengi.

DARASA AISIMAMISHA ILALA KWA SHOO KALI
Reviewed by Erasto Paul
on
December 28, 2016
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili