VIDEO;Mtazame Ng’ombe pori aliyezaliwa na vichwa viwili.

Tumezoea kusikia binadamu wanazaliwa wakiwa wameungana vichwa au muda mwingine mapacha wawili kuungana tumbo, lakini hii ya ng’ombe pori kuzaliwa akiwa na vichwa viwili imekuwa ya tofauti na ya kipekee duniani.

Ndama mmoja huko nchini Pakistani amezaliwa na vichwa viwili katika malisho ya Lucky Foods Dairy Farm mjini Karachi.

Zizi la Lucky Foods Dairy Farm ambako ndama huyo wa maajabu amezaliwa.

Ndama huyo ana vichwa viwili, macho manne, masikio manne, midomo miwili amepatwa na hali hiyo ambayo kitaalamu inaitwa (polycephaly) na inatokea kwa wanyama tuu na huenda hii ni mara ya kwanza kwa ng’ombe pori wa namna hiyo kuzaliwa duniani.

Mwaka jana ng’ombe anayefanana na huyo alizaliwa huko nchini Georgia lakini vichwa hivyo vilikuwa vina masikio matatu na tofauti kidogo na ndama huyu.

Ndama huyo aliyezaliwa septemba 27 mwaka huu kwa sasa analishwa maziwa kwa njia ya kawaida kutokana na kushindwa kunyanyua vichwa vyake viwili na kunyonya moja kwa moja kutoka kwa mama yake.

Tazama video ya mtoto huyo wa ng’ombe pori (Mbogo) mwenye vichwa viwili

VIDEO;Mtazame Ng’ombe pori aliyezaliwa na vichwa viwili. VIDEO;Mtazame Ng’ombe pori aliyezaliwa na vichwa viwili. Reviewed by Erasto Paul on October 04, 2017 Rating: 5

No comments:

Thank you for commenting to Mwanauswahili

Powered by Blogger.