Katibu Mkuu
wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo ameahidi kuwa wizara
yake itakuwa mfano bora wa kumsaidia Rais John Magufuli ili apate kura za
kutosha bila kufanya kampeni mwaka 2020.
Profesa
Mkumbo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wawakilishi wa viongozi wa
mamlaka 19 za maji kuhusu mipango mbalimbali ya kuboresha sekta ya maji nchini.
Amesema
ahadi yake haitakwenda bure kwani mwaka 2020 Rais Magufuli ataanzia Dar es
Salaam hadi Kigoma akipunga mkono tu bila kusema neno lakini kura zitakuwa za
kishindo.
Katibu
huyo amesema Wizara ya Maji ndiyo kila kitu kwani inawagusa wananchi wa hali ya
chini na juu na ndiyo maana kuna ulazima wa kuwa na usimamizi wa kutosha.
Kutokana
na hilo Profesa Kitila amekemea tabia ya vyama vya wafanyakazi kutengeneza
majungu ya wivu na kugeuza mamlaka za maji kuwa vichaka vya majungu na umbea
ambapo matokeo yake ni kuumiza na kuwabambikizia tuhuma viongozi wakiwemo
wakurugenzi wa mamlaka hizo.
Amewataka
wafanyakazi kupigania haki zao huku wakitimiza wajibu wao kwani bila wao
kufanya kazi kwa tija hawawezi kuwa na haki ya kudai maslahi bora.
Katibu wa
kikao hicho Robert Chilewa amesema mamlaka hizo zimekuwa na changamoto kubwa
kutokana madeni yanayofikia Sh 15 bilioni kutoka taasisi na mashirika ya umma.
Amesema
mamlaka zimeanza kuyumba kwa utendaji kazi kutokana na kuondolewa kwa watumishi
wasiofikia elimu ya kidato cha nne ambao walikuwa nguzo imara huku Wilaya ya
Wanging'ombe anakotoka Waziri wa Maji ikiwa na watumishi asilimia 72 wote wa
darasa la saba na akamwomba Profesa Kitila awasaidie watumishi hao warudishwe
kazini.
Profesa Kitila kumsaidia Rais Magufuli apate kura bila kampeni 2020
Reviewed by Erasto Paul
on
October 01, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili