Unaweza ukajiuliza kuwa kuna uwezekano wa mtu wa kawaida kumuoa mtoto
wa Mfalme wa Swaziland, Mswati (III) ajulikanaye kwa jina la Princess
Sikhanyiso.
Ukweli ni kwamba uwezekano huo upo kwa kila mtu ila kwa kigezo kimoja kikubwa cha kutoa ng’ombe 300 kama posa kwa familia hiyo.
Vigezo hivyo vimekuja kujulikana baada ya kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Mzwakhe Phiri mwezi agosti mwaka huu mwenye asili ya Malawi kupeleka posa ya ng’ombe 50 kwa ajili ya kumuoa mtoto huyo wa kifalme.
Mzwakhe Phiri (30) amesema alijua fika kuwa ng’ombe 50 na pesa kidogo walizopeleka kwenye familia hiyo zingewashawishi kumuozesha binti yao lakini mambo hayakwenda kama alivyopanga.
Taarifa kutoka kwenye mtandao wa gazeti la Citizen la Afrika Kusini zinaeleza kuwa mwanaume huyo maombi yake yalikataliwa baada ya kaka zake na Mfalme Mswatii kutaka mahali ya n’gombe mia tatu.
Princess Sikhanyiso (30) ni binti wa kwanza wa Mfalme Mswati aliyezaa na mke wa kwanza, Inkhosikati LaMbikiza na amesomea masuala ya mawasiliano nchini Uingereza na Australia katika ngazi ya Masters.

Pesa sio ishu! timiza kigezo hiki umuoe binti wa Mfalme Mswati
Reviewed by Erasto Paul
on
October 06, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili