Same.Imeelezwa kwamba idadi kubwa ya wanaume hawana uwezo wa kuzaa kutokana na utumiaji wa dawa za kulevya kwa muda mrefu ikiwemo mirungi na bangi.
Kutokana na hali hiyo Mbunge wa Same Mashariki Naghenjwa
Kaboyoka, amemwomba Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kuingilia
kati ili kuokoa vijana.
Kaboyoka amesema wananchi wengi wanajishughulisha na ulimaji
wa zao hilo bila kuogopa sheria hususan za mamba vunta na Gonja.
Amesema sababu ya ulimaji na utumiaji wa bangi na mirungi ni
kutokuwepo kwa kituo cha polisi katika maeneo hayo.
Amesema ameshaongea na Waziri Nchemba ambaye na amemuahidi
kujenga kituo cha polisi katika maeneo hayo
ili kupunguza ulimaji wa mirungi na bangi lakini ni mwaka sasa
umeshapita.
“Nikiwa katika bunge la mwisho niliongea na Katibu Mkuu wa
Mambo ya Ndani kwamba ulimaji wa mirungi, bangi pamoja na uhalifu ni mkubwa na
unazidi kushika kasi katika tarafa hizo."amesema Kaboyoka
Kaboyoka amesema usafiri wa kwenda kuripoti matukio ya
kihalifu ni changamoto ya usafiri ambapo basi linatoka saa nane usiku hadi
kurudi kesho yake.
“Sasa fikiria wahalifu watapelekwaje ,na nani atenda kuripoti
na basi linaloondoka sa nane, hivyo uhalifu unazidi kuongezeka kutoka na kwamba
hakuna wakuwakamata”amesema Kaboyoka.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya hiyo,Sospeter Magonera amesema
wanapinga vikali kilimo hicho cha mirungi kutokana na kwamba kipo kinyume na
sheria za nchi.
“Kilimo hicho kinachangia kwa asilimia kubwa kuharibu nguvu kazi ya
jamii pamoja na nguvu kazi ya Taifa hali ambayo inarudisha maendeleo ya taifa
nyuma”amesema Sospeter
Hata hivyo,diwani wa kata ya mamba miamba, Michael Mauya amesema
uvutaji wa bangi na utumiaji wa mirungi umechangia kwa asilimia kubwa vijana
kuishiwa nguvu za kiume hali ambayo imechangia kupungua kwa idadi ya watoto
katika tarafa hizo.
WANAUME WASHINDWA KUZALISHA KWA SABABU YA MIRUNGI SAME
Reviewed by Erasto Paul
on
September 29, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili