VIGOGO WA ALMAS ‘MAJI YA SHINGO’ KISUTU

 http://mwanahalisionline.com/wp-content/uploads/2017/07/DFGgOlSXkAEqrZF.jpg
UPELELEZI wa kesi kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Shilingi bilioni mbili inayowakabili vigogo wa madini ya almas umekamilika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, anaandika Faki Sosi.

Watuhumiwa katika kesi hiyo ni mkurugenzi wa tathmini wa madini ya almas, Archard Kalugendo (49) na mtathmini wa madini, Edward Rweyemamu (50) wote wakiwa ni wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini.

Upande wa mashtaka umedai mahakamani hapo kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika kwa sehemu kubwa.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage Wakili wa Serikali Paul Kadushi ameeleza kuwa sehemu kubwa ya upelelezi wa kesi umekamilika, hivyo wanaomba kupangiwa tarehe nyingine.

Hata hivyo, wakili wa utetezi, Nehemiah Nkoko alidai kuwa wamewasilisha maombi ya dhamana katika mahakama ya mafisadi.

Baada ya kueleza hayo, hakimu Mwijage ameahirisha kesi hiyo hadi October 12/2017 mwaka huu.

Kwa pamoja watuhumiwa wakabiliwa na kosa moja la kuisababishia Serikali hasara, wanadaiwa kutenda kosa hilo wamelitenda kati ya August 25 na 31/2017 katika maeneo ya Dar es Salaam na Shinyanga.

Source.Mwanahalisi Online
VIGOGO WA ALMAS ‘MAJI YA SHINGO’ KISUTU VIGOGO WA ALMAS ‘MAJI YA SHINGO’ KISUTU Reviewed by Erasto Paul on September 29, 2017 Rating: 5

No comments:

Thank you for commenting to Mwanauswahili

Powered by Blogger.