Waziri wa maji na Umwagiliaji na Mbunge wa
Jimbo la Wanging'ombe Mhandisi Gerson Lwenge Amemuagiza Mkuu wa Wilaya
ya Wanging'ombe Kwenda Kufuatilia Malalamiko ya Wananchi wa Kata ya
Uhambule Juu ya Madai ya Matumizi Mabaya ya Fedha za Ujenzi wa Kituo Cha
Afya Cha Kata Hiyo.
Wakazi Hao Wametoa Malalamiko Hayo Wakati
wa Ziara ya Mbunge wa Jimbo Hilo Mhandisi Gerson Lwenge Alipofika Katika
Kijiji Cha Uhambule Kwa ajili ya Ziara ya Kutembelea na Kukagua
Shughuli za Maendeleo na Kwamba Wanashindwa Kufahamu Ziwapi Fedha Zao
Ambazo Walichanga Kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo Cha Afya.
Wamesema Walichangia Shilingi Milioni Nane
Ambazo Zilipaswa Kutumika Katika Ujenzi wa Kituo Hicho Ambacho Hata
Hivyo Kilivunjwa Kutokana na Kujengwa Chini ya Kiwango na Kuilazimu
Halmashauri Kupeleka Fedha Nyingine Kwa ajili ya Ujenzi Huo.
Kutokana na Malalamiko Hayo Ambayo
Yameonekana Kumtaka Waziri Lwenge Kuchukua Hatua Ngumu Juu ya Suala Hilo
Amelazimika Kumuagiza Mkuu wa Wilaya Hiyo Mohamed Ally Kassinge
Aliyewakilishwa na Katibu Tarafa Bi.Frola Nyato Kulifuatilia na Kumpa
Taarifa Haraka Iwezekanavyo.
Mbunge Lwenge Amesema Haiwezekani Wananchi Wakachanga Fedha ZaoHalafu Zikatafunwa na Baadhi ya Viongozi Wabadhilifu Katika Serikali Hii Inayowapigania Wanyonge.
Hata Hivyo Amesema Endapo Kutabainika Kuwepo Kwa Udanganyifu Katika Fedha Hizo Basi Atatoa Maelekezo Kwa Mkuu Huyo wa Wilaya.
WAZIRI WA MAJI AMUAGIZA DC WANGING'OMBE KUFUATILIA UCHAKACHUAJI WA FEDHA ZA KITUO CHA AFYA
Reviewed by Erasto Paul
on
August 24, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili