Anaitwa Sakina Emmanuel
(20) jina la sanaa ni Skyler,ni
Mwanachuo akisomea Sanaa ya Uandishi wa
habari na Utangazaji katika chuo kimoja
kilichopo Mjini Njombe.
Licha ya kukabiliwa na
masomo hayo ya sanaa pia ni mwanamitindo anayechipukia kutoka Mkoa wa Njombe.
Tayari kazi yake ya
kubuni mavazi imeshaanza kuonekana kwani baadhi ya wananchi Mjini Njombe
wameshaanza kutumia bidhaa anazozalisha kwa mikono yake.
Umri wake wa miaka 20
unaonekana ni mdogo ukilinganisha na mipango mikubwa aliyonayo.
Sakina anasema
anatamani kuona ndoto yake ya kuifikia jamii kwa kiwango kikubwa inafakiwa
kwani sio kupitia sanaa pekee lakini pia anampango wa kuwatembelea wanafunzi wa
kike katika shule mbalimbali za Sekondari zinazopatikana katika Mji wa Njombe
akiwa na lengo la kupiga nao story na kuwaeleza namna gani wanaweza kufikia
maelengo yao.
Anasema watoto wakike
wanakabiliwa na matatizo mengi kutokana na uwepo wa wanafunzi wengi waliokosa
semina elekezi juu ya Elimu Rika katika maswala ya Matumizi ya Pedi wakati wa
kujisitiri katika mizunguko ya siku za Hedhi.
Sakina tayari
ameshaanza kufanya harakati za kupata vibali vya kufanya shughuli hiyo kutoka mamlaka za Serikali huku changamoto
kubwa inayomkabili ni kukosa ufadhili.
Hivi Karibuni Bi Sakina
akiwa katika Kipindi cha Kachumbari
kinachorushwa na kituo cha Redio Kings Fm alisikika akieleza dhamira
yake ya kweli juu ya namna atakavyofanikiwa mpango huo wa kuisaidia jamii.
Anasema japo hataweza
kutoa misaada ya kifedha lakini anaamini ujumbe kupitia elimu anayotarajia
kuitoa utakuwa na chachu hata katika masomo ya wananfunzi hao wa kike.
Katika mahojiano na
kituo hicho pia aliwaomba wadau na wale watakaoguswa kumuunga mkono katika
kufanikisha malengo yake.
Picha hapa chini zinamuonyesha akiwa amevalia baadhi ya Mavazi aliyobuni Yeye Mwenyewe.
Mwandishi;Erasto Mgeni.
Mwanamitindo na Mbunifu wa Mavazi Kutoka Njombe.
Reviewed by Erasto Paul
on
August 23, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili