Shirika la Afya Duniani, WHO, limetoa
tahadhari kuwa, dawa zinazotumika kutibu ugonjwa wa zinaa wa kisonono, zimeanza
kupata usugu na huenda zisiweze kutibu tena ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa
utafiti uliofanywa katika mataifa 77 tofauti Duniani, WHO imebaini kuwa dawa za
kisonono zimeshindwa kutibu ugonjwa huo katika nchi za Japan, Ufaransa na
Uhispania.
Hata hivyo,
shirika hilo linasema wengi wanaoambukizwa ugonjwa huo wako katika nchi
masikini ambazo zina vifaa duni vya kudhibiti ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa
WHO wanaofanya mapenzi bila kinga wapo katika hatari kubwa ya kupata maambukizi
ya ugonjwa huo.
WHO yatahadharisha dawa za kutibu kisonono kushika usugu
Reviewed by Erasto Paul
on
July 07, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili