Wananchi Wangingo’mbe-Njombe Walia na Huduma ya Maji katika Kituo Cha Afya.



Mwandishi;Prosper Mfugale.

Mhariri;Erasto Paul

Kukosekana kwa Huduma ya maji ya uhakika katika kituo cha afya cha Wangingo’mbe Mkoani Njombe Ni moja ya changamoto inayokikabili kituo hicho na kusababisha wananchi kutopata huduma  stahiki za afya.

Imeeelezwa Kuwa katika kipindi ambacho maji yanakosekana basi uongozi wa kituo hicho hulazimika kukifunga kwa muda mpaka pale maji yatakapo patikana kwa njia mbadala.

Wakazi wa kijiji cha Wangingo’mbe wakizungumza na Kings Habari wamesema kutokana na kukosekana kwa maji kituo kinakumbwa na uchafu hasa katika maeneo ya vyoo na vyumba vya kujifungulia akina mama.

Kufuatia Kadhia hiyo wananachi hao wameitaka Serikali kuipa kipaumbele huduma ya maji  kabla ya kuanzisha  huduma ya upasuaji.

‘’Na hawawezi wakakuzalisha kama hakuna maji ina mana una zaa kama kuna maji na kama maji hayapo unaambiwa muuguzi uliyopo njee tunaomba ukasombe maji mahala popote ili uweze kuhudumiwa Yule mgonjwa wako’’alisema mwananchi mmoja.

Image may contain: 3 people, people standing and suit Diwani wa kata hiyo Geofrey Nyagawa amesema changamato hiyo inawatesa wananchi lakini kunamaandalizi ya ujenzi wa Tank kubwa la maji kukabiliana na changamoto hiyo

‘’pamoja na changamoto iliyopo sasa mradi  kubwa wa Wangiwasa umeendelea kuchukua hatua za kutatua hiyo changamoto na limeshajengwa tenki kubwa kwaajili ya kutatua changamoto hii ya maji kwahiyo ninauhakika kwamba sio muda mrefu changamoto ya maji itakuwa imeondoka’’alisema Diwani Geofrey Nyagawa.
 
Image may contain: 2 people, people standing, suit and outdoor
Naibu waziri Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto Dr Hamisi Kigwangala Akiwa Katika ziara yake ya kikazi mkoni Njombe Pamoja na mambo mengine amepokea malalamiko ya wananchi.

Moja ya jambo ambalo wananchi wamewasilisha mbele ya  Naibu waziri ni juu ya kitendo cha mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya kuliondoa gari la wagonjwa huku mkurugenzi akiagizwa kulirudisha haraka.

‘’Hilo Gari lirudi Wangingo’mbe,Saa Nyingine  huwa tunavuruga mambo kwa kutokuwa makini tu kwenye vitu vidogovidogo’’alisema Kingwangala na Kuongeza ‘’watu walishapewa gari wanalijua ni gari lao,wakajenga sehemu ya kulitunza,leo mnaliondoa si kunzisha ugomvi bure tu’’

 Image may contain: 1 person, standing
Wananchi Wangingo’mbe-Njombe Walia na Huduma ya Maji katika Kituo Cha Afya. Wananchi Wangingo’mbe-Njombe Walia na Huduma ya Maji katika Kituo Cha Afya. Reviewed by Erasto Paul on July 19, 2017 Rating: 5

No comments:

Thank you for commenting to Mwanauswahili

Powered by Blogger.