Viongozi
na wanachama 51 wa Chadema waliokamatwa jana wakiwa kwenye kikao cha ndani
wilayani Chato wanaendelea kushikiliwa na polisi kwa mahojiano.
Miongoni
mwa waliotiwa mbaroni wanaoendelea kusota mahabusu ni pamoja na Mwenyekiti wa
Chadema Mkoa wa Geita, Fabian Mahenge na Katibu wake, Sudi Kanganyala.
Mwenyekiti
wa Serikali kijiji cha Mkuyuni, Anaclet Twegosora, ambaye pia ni Mwenyekiti wa
chama hicho Kata ya Chato, amewataja viongozi wengine wanaoshikiliwa kuwa ni
mwenyekiti wa Baraza la Wazee mkoani Geita, Vitus Makange na Neema Chozaire
ambaye ni Mwenyekiti wa Bavicha mkoa.
Wengine ni
Kaimu Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Chato, Uhuru Selemani, Katibu wake
Mangesai Rudonya na diwani mstaafu kata ya Muganza, Marko Maduka.
Kama
ilivyokuwa jana, hakuna kiongozi wa Jeshi la Polisi anayekuwa tayari
kulizungumzia suala hili.
Wakati
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Chato, Alex Mkama, ambaye tukio hilo linaendelea
wilayani kwake akisema hawezi kulizungumzia, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,
Mponjoli Mwabulambo, amesema yuko likizo na kuelekeza atafutwe kaimu wake Allan
Bukumbi ambaye tangu jana hapokei simu yake ya kiganjani wala kujibu ujumbe
mfupi wa maneno anaotumiwa.
Makamu
Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Ziwa Victoria, Ansbert Ngurumo, amesema
kutawanywa kwa mabomu ya machozi na kukamatwa kwa viongozi na wanachama hao
ambao walikuwa katika mkutano wa ndani ni kinyume cha sheria kwa sababu vikao
vya ndani havihitaji kutoa taarifa wala kibali cha polisi kwa mujibu wa sheria
namba 5 ya vyama vya siasa ya mwaka 1995.
Wana Chadema 51 mbaroni Chato
Reviewed by Erasto Paul
on
July 08, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili