Mkazi mmoja wa kitongoji cha Nyambwanda kilichopo katika Kijiji cha Hanga wilayani Kibiti aliyetambulika kwa jina la Hamis Ndikanye (54) ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Jumamosi akiwa nyumbani kwake.
Kwa mujibu
wa maelezo ya ndugu wa marehemu alijitambulisha kwa jina la Hamis Saidi amesema
watu kama watano wakiwa na bunduki walifika nyumbani kwa ndugu yake saa 6
usiku, kisha kufanya mauaji hayo.
Alisema
kabla ya kufanya mauaji hayo walimfunga mke wa marehemu kitambaa usoni na kisha
kumpiga risasi mbili mume wake.
Mganga wa
Kituo cha Afya Kibiti Dk Sadock Bandiko amesema Ndikaye amepigwa risasi mbili
mwilini mwake, moja kichwani na nyingine mgongoni.
Kamanda wa
Polisi mkoa wa Kipolisi wa Rufiji, Onesmo Lyanga, amesema polisi wamekwenda
eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi.
Auawa kwa risasi Kibiti
Reviewed by Erasto Paul
on
July 08, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili