Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezitoza faini kampuni zote za simu kwa kusajili laini bila vitambulisho na kutofuata utaratibu.
Kampuni
zilizotozwa faini hiyo na kiwango kikiwa kwenye mabano ni Airtel (Sh1.08
bilioni), Smart (Sh1.3 bilioni), Vodacom (Sh945 milioni), Zantel (Sh105
milioni) na Halotel (Sh1.6 bilioni).
Mkurugenzi
wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema leo (Julai 14) kuwa hii si mara ya
kwanza kwa watoa huduma hao kukiuka sheria.
Kiliba
amesema kutokana na kurudia kosa hilo, TCRA imezitoza kampuni hizo faini ambazo
Airtel imetozwa Sh542 milioni, Smart (Sh37 milioni), Tigo (Sh625 milioni),
Zantel (Sh52 milioni) na Halotel (Sh822 milioni).
Pia,
kampuni hizo zimetozwa Sh500 milioni kila moja kwa kosa la kuathiri na
kuhatarisha usalama wa umma na jamii ya Watanzania kwa kusajili laini bila
kufuata utaratibu.
TCRA yazipiga rungu kampuni za simu
Reviewed by Erasto Paul
on
July 14, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili