Sophia
Juma, mwanafunzi wa St Marry Mazinde Juu ya Tanga ameibuka kidedea katika
matokeo ya kidato cha sita yaliyotangazwa leo Jumamosi, Julai 15, akishika
namba moja kitaifa.
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk
Charles Msonde imeeleza kuwa nafasi ya pili imeshikwa pia na msichana, Agatha
Julius Ninga wa Tabora Girls. Wote walikuwa wakichukua masomo ya mchepuo wa
Sayansi (PCB).
Kadhalika
taarifa hiyo imeeleza kuwa wasichana wameongoza kwa ufaulu ambapo kati ya
wasichana 28,731 (38 asilimia) waliofanya mtihani, waliofaulu ni 27,577 (sawa
na asilimia 97.21).
Walioshika kumi bora masomo ya Sayansi
1.
Sophia Richard- St Marrys Mazinde
Juu(PCB)
2.
Agatha Julius –Tabora Girls(PCB)
3.
Nathanael Philemon-Mzumbe(PCB)
4.
Mugisha Reynold-Feza Boys(PCB)
5.
Innocent Beda- St Marry Goreti(PCM)
6.
Paschal Masaba-Kibaha(PCM)
7.
Arsen Mwantuke-Marian
Boys(PCM)
8.
Atuganile Cairo- Feza Girls (PCM)
9.
Donel Chihoma- Marian Boys([PCM)
Jumla ya
watahiniwa 75, 116, walifanya mtihani huo Mei mwaka huu.
Kwa
upande wa watahiniwa wavulana, waliofaulu walikuwa ni 42,975 (sawa na asilimia
95.34) kati ya 46,385.
“Mchanganuo
wa ufaulu katika madaraja unaonyesha kuwa watahiniwa walipata daraja la
1-11 umepanda kwa asilimia 0.59 kutoka asilimia 93.13 mwaka 2016
hadi 93.72 mwaka huu,” imesema taarifa hiyo na kuongeza;
“Pia
ufaulu katika madaraja kwa upande wa wasichana umepanda ikilinganishwa na
wavulana. Ubora wa ufaulu kwa wasichana ni asilimia 94.07 ikilinganishwa na
asilimia 93.49 ya wavulana.”
Shule zilizoongoza
Katika
matokeo hayo, Shule ya Wasichana ya Feza Girls ya Dar es Salaam imeibuka kinara
kwa watahiniwa wake 67 kufaulu kwa kupata daraja la kwanza na la pili.
Shule
nyingine zilizoibuka kidedea katika matokeo hayo ni Marian Boys (Pwani)
iliyoshika nafasi ya pili, Kisimiri (Arusha) imeshika nafasi ya tatu na Ahmes
(Pwani) imeshika nafasi ya nne.
Shule
nyingine ni Marian Girls (Pwani) iliyoshika nafasi ya tano,
Mzumbe (Morogoro) nafasi ya sita, St Marry Mazinde Juu (Tanga) nafasi ya saba,
Tabora Boys (Tabora) nafasi ya nane, Feza Boys (Dar es Salaam) nafasi ya tisa
na Kibaha ya Pwani iliyoshika namba kumi.
Shule zilizoshika mkia
Shule
zilizoshika mkia ni Kiembesamaki ya Unguja, Hagafilo (Njombe), Chasasa (Pemba),
Mwenyeheri Anuarite (Dar es Salaam) na Ben Bella (Unguja). Nyingine zilizotajwa
kushika mkia ni Meta (Mbeya) na Mlima Mbeya (Mbeya).
Nyingine
ni Shule ya Sekondari ya Al-Ihsan Girls (Unguja) na St Vicent(Tabora).
Waliofutiwa matokeo
Kadhalika
taarifa ya Necta imeeleza kuwa watahiniwa 10 walifutiwa matokeo kwa makosa ya
kufanya udanganyifu.
Taarifa ya
Dk Msonde imeeleza kuwa kati ya watahiniwa hao kumi, saba ni wa shule na watatu
ni wa kujitegemea.
Pamoja na
hao kumi, watahiniwa wengine 15 hawakufanya mitihani ya baadhi ya masomo
kutokana na matatizo mbalimbali ikiwamo ya kiafya na hivyo kushindwa
kufanya mitihani hiyo.
‘Watahiniwa
hao wamepewa fursa ya kufanya mitihani ya kidato cha sita, Mei 2018 kama
watahiniwa wa shule,” imesema taarifa ya Dk Msonde.
Pia, wapo
watahiniwa 69 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya
mitihani yote yote, wamepewa fursa ya kufanya mitihani hiyo, Mei 2018.
Sophia Juma aongoza taifa matokeo kidato cha sita
Reviewed by Erasto Paul
on
July 15, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili