Kanisa
Anglikana Tanzania linakusudia kufanya mabadiliko ya katiba yake ili kuruhusu
kanisa kufanya uwekezaji.
Akizungumza
wakati wa ibada iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Albano jijini Dar es
Salaam leo, Askofu Mkuu wa kanisa hilo nchini, Dk Jacob Chimeledya amesema
lengo la mabadiliko hayo ni kulifanya kanisa kugusa maisha ya watu.
Dk
Chimeledya amesema kanisa hilo linaunga mkono jitihada za Rais John Magufuli za
kuwainua watu wa chini na kwamba, jambo hilo haliwezi kufanikiwa kama injili
haitawafikia.
"Nguvu
ya kanisa lazima iguse maisha ya watu wa chini. Tutafanya mabadiliko ya katiba
ili kuruhusu uwekezaji ambao tulishaanza kuufanya," amesema Dk Chimeledya.
Askofu
Chimeledya amewataka mapadri wa kanisa hilo kufanya jitihada za kuanzisha
parokia zingine katika maeneo yao kwa sababu Dayosisi ya Dar es Salaam ina
parokia chache ambazo hazifiki 100.
Katiba ya Kanisa la Anglikana kubadilishwa
Reviewed by Erasto Paul
on
July 16, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili