Dar es Salaam. Mfanyabiashara
Yericko Nyerere amefikishwa leo (Ijumaa) katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu na kupandishwa kizimbani akikabiliwa na kesi nyingine ya kuchapisha
maneno yenye nia ya uchochezi kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.
Akisomewa shtaka na Wakili wa Serikali Mwandamizi,
Kishenyi Mutalemwa kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage, Yericko
anadaiwa kuwa Mei 28, 2017 kwa nia ya kuwachochea Watanzania alichapisha
maneno kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook yasemayo:
“Maazimio ya Baraza Kuu yalikuwa (1) Katiba Mpya,
(2) Tume Huru, (3) Bunge, (4) Haki ya Kikatiba ya kuishi (Ben Saanane), (5)
Haki ya Kikatiba ya kukutana na kuzungumza (Mikutano ya Hadhara ya Kisiasa)
Hayo ndiyo yatahubiriwa katika Operesheni Ukuta.
Baraza Kuu limeridhia kwa kauli moja kwamba vita rasmi ya
kulikomboa Taifa imezinduliwa na kama wewe Mtanzania unaogopa kulitetea Taifa
hili ni bora uka kaa kando, nenda huko CCM ambako michemsho na supu vipo kwa
wingi…kufa kwetu ni ukombozi wa Tanzania….” Mwisho wa kunukuu.
Yericko ambaye anatetewa na Wakili Peter Kibatala baada
ya kusomewa shtaka hilo amekana na upande wa mashtaka umedai kuwa
upelelezi wake bado haujakamilika.
Hakimu Mwijage amemtaka mshtakiwa huyo kuwa na mdhamini
mmoja ambaye amesaini hati ya dhamana ya maneno ya Sh10 milioni, amekamilisha
na kuachiwa huru. Kesi imeahirishwa hadi Julai 6, 2017 kwa ajili ya kutajwa ili
kuangalia upelelezi utakuwa umekamilika ama la.
Yericko Nyerere apandishwa tena kizimbani
Reviewed by Erasto Paul
on
June 09, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili