IMENDIKWA NA HILALI DAUDI, GABRIEL NG’OSHA NA GLADNESS MALLYA |AMANI
ARUSHA: Siku nne baada ya kutokea kwa ajali iliyosababisha vifo vya wanafunzi 32, walimu wawili na dereva mmoja wa Shule ya Lucky Vincent Nursery and Primary ya jijini hapa iliyotokea katika Mlima wa Rhotia kuelekea mjini Karatu, mazito yameibuka kutoka eneo la ajali, Gazeti la Amani limesheheni.
Majeneza ya miili ya marehemu hao.
Tangu kutokea kwa ajali hiyo mambo mbalimbali yamekuwa yakisemwa juu
ya eneo hilo la ajali ikiwemo madai ya kuwapo kwa jini msababisha ajali
au mtoa roho za watu hivyo Gazeti la Amani lililazimika kufika mahali hapo ili kupata majibu kamili.Kabla ya kuweka kambi eneo hilo mapema wiki hii, Gazeti la Amani lilipokea madai mengi kutoka kwa vyanzo mbalimbali ikisemekana kuwa eneo hilo lina jini ambaye amekuwa akisababisha ajali nyingi.
Baadhi ya madaftari ya watoto hao.
AJALI TATU KWA SIKU MOJAVyanzo hivyo vilidai kuwa, mwezi Januari, mwaka huu, kulitokea ajali tatu tofauti kwa siku moja. Ilidaiwa kuwa, ajali ya kwanza ilitokea asubuhi, ya pili mchana na nyingine alasiri.
KUWEPO KWA HARUFU YA DAMU
Mbali na ajali hizo, pamoja na mvua kubwa kunyesha eneo la tukio, lakini bado wanakijiji wamekuwa wakisikia harufu ya damu inayotokana na ajali zilizowahi kutokea eneo hilo.
Mwandishi wa Gazeti la Amani, Hilali Daudi akiwa eneo la tukio.
KUTOKUWEPO KWA DAMUMoja ya swali ambalo wengi wamekuwa wakijiuliza ni kutokana na eneo la ajali hiyo kutokuwa na damu kama ambavyo ajali nyingine zilizowahi kutokea, jambo linalowafanya watu kuamini kuwa kuna jini msababisha ajali ambaye amekuwa akilamba damu za watu wanaokata roho eneo hilo.
DEREVA APIGWA MWANGA MKALI
Mmoja wa madereva wa barabara hiyo ya Arusha- Karatu alifunguka kuwa, kuna siku akiwa anafanya safari yake kama kawaida, majira ya usiku alishangaa kumulikwa na mwanga mkali kama wa tochi, lakini alipofi ka eneo la tukio hakuona mtu yeyote aliyemmulika na kama asingekuwa makini basi angeweza kutoka barabarani na kutumbukia korongoni.
Gari likipita barabarani karibu na eneo la tukio.
DEREVA AVUTWA KIMIUJIZADereva mwingine alidai kuwa, kuna siku akiwa anapita eneo hilo, alishangaa kuona gari linavutwa kuelekea korongoni, lakini jamaa huyo alijiongeza kwa kuchukua tahadhari lasivyo anadai angepoteza maisha kwa kutumbukia korongoni.
AMANI LATINGA ENEO LA TUKIO
Kutokana na sintofahamu ya baadhi ya watu mbalimbali kudai kuwa, ajali ile inahusishwa na masuala ya majini au mizimu, Gazeti la Amani lilifunga safari hadi eneo la tukio mjini Karatu na kuzungumza na viongozi na baadhi ya wanakijiji kuhusu minong’ono hiyo.
Mwenyekiti wa Kijiji, Patrice Sarya
MWENYEKITI WA KIJIJIPatrice Sarya, ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Marera Kata ya Rhotia wilayani Karatu ambaye alidai kuwa, eneo hilo halina mambo yoyote ya mizimu wala majini zaidi ya kutokea kwa ajali kama ajali zingine.
Mtendaji wa Kijiji, Bura I Bura akizungumza na Global TV Online pamoja na Gazeti la Amani.
MTENDAJI WA KIJIJIGazeti la Amani lilikwenda mbele zaidi na kuzungumza na mtendaji wa kijiji hicho, Bura I Bura ambaye naye alidai kuwa, si kweli kwamba eneo hilo limekuwa na ajali za kishirikina au kimajini.
“Mimi ni mwenyeji wa eneo hili kwa muda mrefu sana, si kweli kwamba eneo lililotokea ajali huwa lina ajali nyingi kama watu wanavyosema na hakuna ajali ya majini au ushirikina,” alisema Bura.
WASIKIE WANAKIJIJI
Gazeti la Amani liliwatafuta wanakijiji wa eneo hilo ambao walikubali kuzungumza kwa sharti la kutokupigwa picha wala kutaja majina kwa sababu zao binafsi.
Mitihani ya wanafunzi hao.
HAKUNA ALAMA ZA BARABARA“Mimi ni mkazi wa kijiji hiki, ni kweli hili eneo ni hatari sana, lakini hakuna vibao vya alama za barabarani zinazoonesha chochote,” alisema mmoja wao.
ALAMA YA SPIDI 50 YAWEKWA
“Baada ya tukio hilo la ajali, ndiyo kuliwekwa kibao cha kuonesha kuwa mwisho wa spidi katika eneo hilo ni spidi 50 kwa saa.
Namba ya gari lililopata ajali.
AJALI YA MCHUNGAJI NA NG’OMBE WAKE“Mimi kama mwanakijiji wa eneo hili nakumbuka ajali siyo nyingi sana eneo hili, ajali ya mwisho ilikuwa mwaka jana ambapo mchungaji wa mifugo aligongwa na gari wakati anavusha ng’ombe wake, yeye na wale ng’ombe kumi wote walifi a palepale.
MAALIMU HASSAN AFUNGUKA
Akizungumza na gazeti hili juu ya tukio hilo, Mtabiri Maalim Hassan Yahaya, yeye alidai kuwa alitabiri baadhi ya matukio ambayo yatatokea na yanaendelea kutokea nchini yakihusishwa na vyombo mbalimbali vya moto.
“Mwezi Januari, mwaka huu nilitabiri kuwa kutakuwa na matukio mengi sana yatokanayo na vyombo vya moto na kwa mujibu wa nyota, mwezi Mei ndiyo mwezi wa kwanza kwenye mwaka kwa hiyo matukio yataendelea kutokea hadi mwezi wa tisa.
“Matukio yatahusisha sana watoto, iwe kwa ubaya au uzuri na ndiyo maana hata rais mpya wa Ufaransa, Emmanuel Macron ni kama mtoto kulingana na viongozi wa awali waliotangulia,” alisema Maalim.
Eneo la Ajali Mazito Yaibuka Karatu, Madereva Wanena
Reviewed by Erasto Paul
on
May 12, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili