Takwimu zinaonesha kati ya
wafungwa 4,815 walionufaika na mpango wa Parole (Wafungwa kupewa vifungo
vya nje) ni wafungwa 25 pekee ambao walikiuka mashart.
Takwimu hizo zimetolewa leo Jijini Dar
es salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Mwigulu Nchemba
wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya Parole na kusema mpango huo una lengo
la kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani na kuisaidia idara ya
mahakama kusikiliza kesi za watuhumiwa kwa uharaka.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Parole
Mhe. Augustine Mrema amesema kazi yake kwa sasa ni kuhamasisha wananchi
waache kufanya vitendo vya kihalifu.
Wakati huohuo waziri Mwigulu
amezungumzia suala la haki ya mtuhumiwa hususani anapokamatwa au
kushikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano,ambapo amesema jeshi la
polisi lina wajibu wa kumuachia huru mtuhumiwa yoyote ambaye anabainika
kutohusika katika tuhuma alizoshukiwa.
“Mwenye Makosa ni vizuri
kufika kwenye mikono ya sheria, lakini mkijiridhisha kwamba hana makosa,
au siyo yeye mliokuwa mnamtafuta, isiwe tabu kumuachia” Amesema Nchemba
Haya ndiyo mafanikio ya vifungo vya nje
Reviewed by Erasto Paul
on
March 22, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili