Jinsi vitambi vinavyosababisha ugumba

Husababisha ugumbs, upungufu wa nguvu za kiume
Husababisha ugumba, upungufu wa nguvu za kiume na shinikizo la damu. 
By Herieth Makweta, Mwananchi; hmakweta@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Baadhi ya watu wamekuwa wakiona vitambi kama sifa za mtu kuwa vizuri kimaisha, lakini sasa vinaweza kuwa majuto kwao baada ya kuelezwa kuwa vina madhara mbalimbali ikiwamo kuumwa magoti, miguu na kupata matatizo ya moyo.
Mtaalamu wa ushauri elimu ya mapishi na sayansi ya jikoni kwa watu wanaosumbuka na magonjwa mbalimbali ya lishe, Dk Boaz Mkumbo alisema sukari nyingi mwilini kwa wanaume hupandisha homoni ya insulin inayovuruga homoni nyingine na kusababisha homoni ya kiume (testosterone) kuharibiwa.
Madhara mengine ni kuharibika mwonekano, kupata ugumba, tatizo la kusahau, kisukari cha ubongo ‘type 3 diabetes’, upungufu wa nguvu za kiume na shinikizo la damu.
 “Homoni hii inajenga misuli, kukupa nguvu na shauku ya ndoa kwa jinsia tofauti inashuka chini ya kiwango, huenda sambamba na kuongezeka kwa estrogen homoni ambazo hupunguza maumbile sehemu za siri,” alisema Dk Mkumbo.
Habari zaidi soma Mwananchi


Jinsi vitambi vinavyosababisha ugumba Jinsi vitambi vinavyosababisha ugumba Reviewed by Erasto Paul on February 22, 2017 Rating: 5

No comments:

Thank you for commenting to Mwanauswahili

Powered by Blogger.