RICHARD BUKOS, RISASI
DAR ES SALAAM:
Mwanamuziki wa Taarab, Mariam Mohammed Uwesu ‘Mariam BSS’ Jumapili
aliyopita alijikuta akimwagiwa kojo wakati wa sherehe ya kumbukumbu ya
siku yake ya kuzaliwa ‘bethidei’ iliyofanyika huko Manzese katika baa
inayojulikana kama Bar Mpya, jirani na Friends Corner Hotel.
Katika
hafla hiyo iliyosindikizwa na Kundi la Taarab la Diamond Classic
Modern usiku huo, mshiriki huyo wa zamani wa shindano la kusaka vipaji
la BSS, alimwagiwa pombe, maji machafu, soda na ndoo ya chooni iliyokuwa
na mikojo wakati wa tukio la kufungua shampeni, ambalo kwa desturi
mpya ya sasa, mhusika humwagiwa kinywaji hicho, sambamba na maji na
vinywaji vingine laini.
Mambo
yalienda vizuri hadi mshereheshaji katika tukio hilo, Mc Andamakopa
alipotangaza kuwa wakati wa kufungua shampeni umefika na mara tu baada
ya kinywaji hicho kufunguli wa, wageni wa alikwa walianza kummwagia kwa
staili ya kumuogesha.
Kitendo
hicho kiliamsha shamra kwa watu waliokuwepo, wakiwemo ‘masela’ ambao
nao walimvamia na kuanza kummwagia vimiminika mbalimbali zikiwemo pombe
kali, soda na maji machafu.
Wakati
hayo yakiendelea, wanaosadikika kuwa masela, walienda chooni na
kuchukua ndoo ya maji yaliyochanganyika na mikojo na kwenda kummwagia
mwilini hali iliyosababisha baadhi ya wasamaria wema kumchomoa katikati
ya kundi hilo baada ya kushtukia harufu kali ya mkojo.
Baada
ya kuchomolewa alikimbizwa chooni kwenda kuoga ndipo mambo mengine
yakaendelea huku mwanamuziki huyo akiwalalamikia waliomfanyia kitendo
hicho akisema hakikuwa cha kiungwana.
“Ukweli suala la kumwagiana shampeni au
maji ni la kawaida, lakini kitendo walichonifanyia cha kunimwagia maji
machafu yanayonuka harufu ya mikojo si cha kiungwana.
“Ile
ndoo wameitoa chooni na si unajua vyoo vya baa, walevi wengine
wakienda kukojoa hawaangalii, wanakojolea hata maji ya kunawa , ”
alilalamika Mariam.
Mwanamuziki maarufu wa Taarabu amwagiwa Mkojo siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa **Happy Birthday**
Reviewed by Erasto Paul
on
January 15, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili