LEO kwenye safu hii tutaongelea jinsi ya
kuifanya ngozi yako kuwa kavu na kung’aa kwa wale wenye mafuta kwa
kutumia toner ya limao na barafu.
Mahitaji
Glasi ya maji
Limao
Kijiko
Tray ya barafu
JINSI YA KUPATA TONER HIYO
Chukua maji masafi, changanya na maji ya
limao kisha koroga kuhakikisha limao na maji vimechanganyika. Baada ya
hapo, weka maji hayo kwenye tray ya barafu kisha weka kwenye friji mpaka
yagande.
Jinsi ya kutumia toner hii Unaweza
kutumia baada ya kuoga, unachukua lile barafu lako lenye limao tayari,
unasugua kwenye ngozi yako.
Kazi yake ni kufungua vitundu vya hewa
na kung’arisha ngozi kwa ujumla. Tumia barafu hilo kabla ya kupaka
makeup. Mbali na kufanya kazi hizo mbili, pia inasaidia kuifanya ngozi
yako kubana.
Nikisema hivyo namaanisha inaepusha
ngozi kulegea, nadhani tumewahi kuona ngozi ikilegea mpaka inaning’inia.
Wengine hupenda kutumia toner hii usiku baada ya kutembea juani kwa
muda mrefu na baada ya ngozi kuchoshwa na make-up za kila siku.
Limao na barafu kwa kung’arisha ngozi
Reviewed by Erasto Paul
on
January 24, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili