Kesi
ya wizi wa simu aina ya Tecno iliyochukua takriban miaka miwili
mahakamani, imefika tamati kwa mtuhumiwa kufungwa maisha jela.
Hukumu
hiyo ilifikiwa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, baada ya
mtuhumiwa Kassim Salum (18) kukutwa na hatia kwa kosa la unyang’anyi wa
kutumia nguvu wa simu yenye thamani ya Sh110,000.
Mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Januari 28, mwaka jana katika Mtaa wa Ghana Magenge eneo la Buguruni jijini Dar es Salaam.
Ushahidi uliotolewa na mashahidi watano uliiwezesha mahakama kukubaliana na madai ya mlalamikaji Lutifia Mohamed.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Flora Haule alisema, “Baada ya kusikiliza mashahidi wote watano wa upande wa jamhuri, mahakama inaona wamethibitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa.”
Akipitia
ushahidi huo, hakimu Haule alisema mshtakiwa alimsukuma mlalamikaji na
kuangukia katika karai la mafuta ambalo lilikuwa jikoni.
Mashahidi
hao waliieleza jinsi mshtakiwa alivyomvamia mlalamikaji akimtaka atoe
simu aliyokuwa nayo na katika purukushani hizo, alimpiga ngumi tumboni
hali iliyosababisha kuishiwa nguvu.
Ilielezwa
kuwa kutokana na kupigwa, mlalamikaji aliirusha simu upande wa pili
ambapo kulikuwa na muuza chipsi, hivyo Salum aliamua kumuachia
mlalamikaji ili aende kuifuata.
Hata
hivyo, wakati mlalamikaji anajaribu kuokota simu yake, Salum alimsukuma
akaangukia katika karai la mafuta ya moto na kumsababishia kuungua eneo
lote la mgongoni. Inadaiwa baada ya hapo Salum alichukua simu hiyo na
kutoweka nayo.
Wakili
wa Serikali, Sylvia Mitanto aliomba mahakama impe adhabu kali Salum ili
aweze kujifunza kwa kuwa amemtia mlalamikaji ulemavu wa kudumu.
Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, mahakama ilitoa nafasi kwa mshtakiwa kujitetea na Salum aliomba isimpe adhabu kali akisema si yeye aliyechukua simu hiyo, bali ni chuki binafsi za mitaani wanakoishi.
Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, mahakama ilitoa nafasi kwa mshtakiwa kujitetea na Salum aliomba isimpe adhabu kali akisema si yeye aliyechukua simu hiyo, bali ni chuki binafsi za mitaani wanakoishi.
Jela maisha kwa kupora simu ya Sh110,000 na kujeruhi
Reviewed by Erasto Paul
on
December 30, 2016
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili