Mwanamume
mwenye miaka 45 Yohana Omari anatafutwa na Polisi kwa tuhuma za
kumlawiti mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 16, kwa zaidi ya
miaka miwili.
Omari
ametoroka baada ya kupata taarifa kuwa anatafutwa na wananchi kutokana
na tukio alilokuwa akimfanyia kijana huyo (jina linahifadhiwa) tangu
mwaka 2013.
Akizungumzia
tukio hilo, kijana huyo alisema kuanzia mwaka huo, akiwa darasa la nne
amekuwa akifanyiwa kitendo hicho na baba yake na kukatazwa asiseme.
Alisema
siku ya kwanza alipobaini anafanyiwa ilikuwa usiku akiwa amelala,
alishtuka kutokana na kuhisi maumivu makali na kumkuta baba yake
amemlalia juu.
Alifafanua
kuwa kuanzia hapo hayo yakawa ndiyo maisha yake na anapolalamika hukosa
baadhi ya huduma, jambo lililokuwa likimlazimu akubali kuendelea kwa
shingo upande.
“Kuna
mafuta huwa ananipaka na kunifanyia kitendo hicho, nimeishi kwa tabu
ikiwamo kuamka asubuhi nimechoka na sina hamu ya jambo lolote, natamani
kulala.
“Imefikia mahali natoka majimaji hadi kuogopa kujichanganya na wenzangu,” alisema kijana huyo.
Kijana
huyo alisema kabla ya kuishi na baba yake, alikuwa anaishi na mama
yake, lakini alipata mwanamume akaolewa kwa sharti la kutokuishi na
yeye, ndipo akampeleka kwa baba yake.
Alieleza kuwa licha ya kuwaeleza ndugu wa familia, wakiwamo bibi zake, hakuna walichomsaidia.
“Nimemaliza darasa la saba, nimechaguliwa kujiunga sekondari, lakini sina uhakika wa kuendelea na masomo.
“Baba amekimbia na kuna viashiria alitumia rushwa, ulinzi shirikishi badala ya kumkamata walimtorosha,” alisema.
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa wa Kwa Mustapha Pugu, Dar es Salaam, Bahati Omari
alisema baada ya kupata taarifa hizo, kwa kushirikiana na vijana wake,
walifikisha taarifa polisi ili akamatwe lakini alikuwa ameshatoroka.
Askari
polisi mmoja wa eneo hilo alisema baada ya kupokea malalamiko hayo,
walimpeleka hospitali kijana huyo kumfanyia vipimo ambavyo alibainisha
kuwa amefanyiwa kitendo hicho mara nyingi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni alisema suala hilo lipo chini ya upelelezi.
“Tumepokea
hayo malalamiko, tunayachunguza kwa sababu yanachanganya, amekuwa
akifanyiwa vitendo hivyo tangu mwaka 2013 na amekuja kubainisha leo,
hivyo inahitaji upelelezi wa kina,” alisema Hamduni.
Baba Adaiwa kumlawiti mtoto wake wa kiume
Reviewed by Erasto Paul
on
December 30, 2016
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili