Instagram wazindua huduma ya video ya moja kwa moja

Mtandao wa Instagram umezindua huduma za matangazo ya moja kwa moja kwa njia ya video.
 160512073910_instagram_logo_640x360_bbc_nocredit
Mtu yeyote anayetazama anaweza kutoa maoni yake kwa kuweka emoji ambazo hujitokeza katika video hiyo ya moja kwa moja. Japo imeonekana kuwa ya kawaida lakini ina tofauti kubwa na huduma ya mitandao mingine kwa kuwa unapomaliza kuweka matangazo yako hupotea kabisa.

Hiyo inamaanisha hutaweza tena kusambaza link ya video yako kwa wanaotazama na hawataweza kuiona tena baada ya video hiyo kupotea.

 Msemaji wa mtandao huo amesema kuwa huduma hiyo inalenga kuwafanya wateja kuhisi furaha na kuweza kusambaza chochote wanachotaka kupitia huduma hiyo.
 http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2016/11/instagram-direct-ephemeral.png
Aidha ameongeza kuwa programu hiyo itaanza kusambazwa kwa kundi la wateja wa mtandao huo kabla ya kuanza kutumika rasmi na kila mtu katika kipindi cha wiki chache zijazo.
Instagram wazindua huduma ya video ya moja kwa moja  Instagram wazindua huduma ya video ya moja kwa moja Reviewed by Erasto Paul on November 25, 2016 Rating: 5

No comments:

Thank you for commenting to Mwanauswahili

Powered by Blogger.