Wabunge wa
Chadema, Joshua Nassari (Arumeru Mashariki), Godbless Lema ( Arusha Mjini) na
Mchungaji Peter Msigwa(Iringa Mjini) wamewasilisha Takukuru ushahidi wanaodai
unaonyesha wa jinsi madiwani wao walivyonunuliwa kwa kupewa rushwa.
Wabunge wao,
wamewasilisha ushahidi huo mchana wa leo Jumatatu kwenye ofisi za Makao Makuu
ya Takukuru zilizopo Upanga Dar es Salaam.
Wabunge
hao wamewasili katika ofisi hizo saa 8.39 mchana na kukutana na waandishi wa
habari waliokuwa wakiwasubiri.
Katika
kile ambacho waandishi hawakukifikiria, wabunge hao waliwasili kwa miguu na kuelekea moja kwa moja ndani
ambapo waandishi walizuiwa kuingia.
Ushahidi
huo, wameuwasilisha ikiwa imepita siku moja tangu Lema na Nassari walipofanya
mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha kueleza jinsi madiwani wao
walivyoshawishiwa na kwa rushwa kuihama Chadema.
VIDEO-Lema, Nassari, Msigwa waingia Takukuru
Reviewed by Erasto Paul
on
October 02, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili