Na Erasto Mgeni,Njombe
PICHA;Naibu waziri wa Nishati na Madini Dokta Medad Kalemani akiwapa
maagizo wakandarasi wanaojenga kituo cha kupoozea umeme Mjini Makambako.Picha
na Erasto Mgeni.
Naibu waziri wa Nishati na Madini Dokta Medadi Kalemani
ameagiza kutofanya malipo ya aina yoyote kwa mkandarasi anayefanya kazi ya
kupanua kituo cha kupoozea umeme
kilichopo Makambako katika utekelezaji wa mradi wa Umeme wa Makambako Songea.
Kituo cha kupoozea Umeme kinajengwa katika Eneo la Makambako
ambacho kitaunganishwa na Mfumo wa usafarishaji Umeme wa Kilomita 250 wenye
msongo wa kilovolt 220 kutoka Makambako Hadi Songea.
Dkt.Kalemani alitoa maagizo ya kuzuia malipo kwa Mkandarasi
anayejulikana kwa Jina la Jv Shandong Taikai Power Eng.Ltd $ Noringo
International Cooperation baada ya
kufanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Mradi na kuona mradi huo unasua sua
kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Kalemani alisema Ni mara yake ya tatu kufika katika kituo
hicho lakini kila anapofanya ziara eneo hilo haoni chochote kinachoendelea
Tangu Mwezi Julai Mwaka jana.
Akizungumza mara baada ya kumaliza ziara yale Alisema‘’Kwa kweli kwa kituo cha Makambako kazi
haijafanyika,nimetoa maelekezo ni matumaini yetu watayafanyia kazi,sasa
nimeelekeza ujenzi uanze mara moja kwa sababu wakandarasi waliondoka site’’Alisema
Kalemani Na Kuongeza ‘’ Lakini Kazi ya
Pili nimezuia sasa wasilipwe kwanza
mpaka kazi waanze,iridhishe iwe verified ndo waweze kulipwa kwa mujibu wa kazi
walizofanya.’’
Licha ya Kuzuia malipo hayo pia Dkt Kalemani alimuagiza mkuu wa mkoa kuhakikisha
mkandarasi huyo hatoki nje ya mkoa wa Njombe mpaka pale atakapojiridhisha
maendeleo ya mradi huo unaotarajia kuwanufaisha wananchi wengi wa mkoa wa
Njombe na Ruvuma.
‘’Nimeomba sana uongozi wa mkoa utusaidie kuwafanya wakae
site,nimeshauri na nimeelekeza meneja wetu awazuie kwanza hiyo Kampuni wasiondoke kwanza kwenye mkoa wa Njombe Mpaka
watakapoanza Shughuli za Ujenzi na Tumejiridhisha’’ Alisema Kalemani
Katika ziara yake ya Kushtukiza Amemuagiza Mkurugenzi mkuu
wa Tanesco kumchukulia Hatua Msimamizi
wa ujenzi wa kituo cha kupoozea na asipo
fanya hivyo basi atalazimika kumchukulia hatua yeye mwenyewe.
Aliagiza pia kubadilishwa kwa msimamizi wa ujenzi wa mfumo
wa usambazaji umeme wa msongo wa kilovolti 33 wenye Jumla ya kilomita 900 kazi
inayofanywa na mkandarasi anayejulikana kwa Jina la Isolux Ingeniera S.A.
Amesema Mkandarasi huyo alitakiwa awe ameshakamilisha kazi
ya kusambazi umeme Tangu Disemba mwaka
jana katika baadhi ya vijiji vya Halmashari
ya Makambako na Njombe ambapo mpaka sasa utekelezaji wa kazi hiyo ni
Asilimia 32.8 pekee.
‘’Kwa Upande wa vile
vijiji 120 ambavyo vinapelekewa umeme na mradi ule nimekuta kazi hazijafanyika
Ipasavyo,kwahiyo tumetoa maelekezo Yule ni msimamizi kwasababu ameshindwa kufanya
kazi vizuri na kwakweli hakuwepo site wakati tunatembelea,sasa huko kokote
alipo atakaporudi awekwe kazi nyingine asisimamie mradi’’Alisema Kalemani
Kitendo cha naibu waziri kufika katika maeneo ya utekelezaji
wa Mradi na kutowaona wakandarasi wakiwa Site kilionekana kumchukiza sana naibu
waziri hali iliyopelekea kuchukua maamuzi hayo ya kuzuia malipo kwa wakandarasi
huku akiwataka kuhakikisha kazi hiyo inamalizika kwa wakati.
Dokta Kalemani alipongeza Kampuni ya Kalpataru Power Transmission
Ltd inayojenga Njia Kuu ya Mfumo wa usafarishaji Umeme wa Kilomita 250
wenye msongo wa kilovolt 220 kutoka Makambako Hadi Songea kwakuwa inaendelea
vizuri na kazi inayofanyika inaonekana.
‘’Mradi wa tatu
unakwenda Viruzi ule wa kusafirisha njia za umeme,ile kampuni ya waindia
Kalpataru wanafanya vizuri,tumewahamasisha tu wasipunguze spidi ili wamalize
ndani ya muda kwasababu wanamaliza Mwezi Marchi’’Alisema Kalemani na kuongeza’’ Kwahiyo nio matarajio yetu kuja kufikia
mwezi Septemba Mwakani mradi wa Makambako-Songea utakuwa umekamilika,wananchi
22,700 wataunganishia umeme na njia za usafirishaji umeme wa kilomita 250
kutoka makambako kupitia madaba mpaka songea zitakuwa zimekamilika’’
Mradi huu wa kutoka
Makambako Songea ni mradi unaofadhiliwa na serikali ya Sweeden kupitia shirika
lake la maendeleo la Sweden pamoja na serikali ya Tanzania kupitia Shirika la
umeme Tanesco.
Mradi huu umekusudia kusambaza umeme vijini ili kuchangia maendeleo ya wananachi katika vijiji na miji iliyopo katika moa wan Jombe na Ruvuma.
Mradi huu umekusudia kusambaza umeme vijini ili kuchangia maendeleo ya wananachi katika vijiji na miji iliyopo katika moa wan Jombe na Ruvuma.
Naibu waziri wa Nishati na madini Dokta Kalemani anaendelea
na Ziara Yake katika mikoa ya Kusini akikagua miradi mbalimbali inayotekeleza
Mpango wa umeme Vijijini Rea awamu ya Tatu.
NAIBU WAZIRI NISHATI DKT. KALEMANI AGHADHABISHWA NA WAKANDARASI MRADI WA UMEME WA MAKAMBAKO-SONGEA.
Reviewed by Erasto Paul
on
August 16, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili