Kwa miaka mingi tulikuwa tunasikia midundo ya ngoma kuashiria kuanza kwa taarifa ya habari kwenye redio ya Taifa RTD na baadae TBC.
Ilikuwa ni midundo maarufu sana na yeyote aliyeisikia hata kwa mbali alijua wazi huu ni wakati wa taarifa ya habari, ila kwa majonzi makubwa midundo hii haipo tena huko TBC.
Midundo hii ni ufundi wa Mzee Morris Nyunyusa mlemavu wa macho aliyekuwa na kipaji cha ajabu cha kupiga ngoma 17 kwa wakati mmoja, na midundo hii ilihusisha ngoma zote hizi.
Umahiri wake huu ulimfanya ajulikane ndani na nje ya nchi huku akipata mialiko mingi tu!, ikiwamo ziara mojawapo aliyowahi kuifanya nchini JAPAN ambapo alipewa mualiko nchini humo.
Katika ziara hiyo mzee Morris aligeuka kuwa kivutio kikubwa mno kwa maonyesho hayo, hata kumfanya mwanamziki nguli bwana Mbaraka Mwinshehe kumtungia wimbo mzee huyu juu ya umahiri aliouonyesha katika tamasha hilo.
Hakika mzee huyu likuwa kivutio cha wageni mbalimbali kutoka mabara mbalimbali, pindi walipokuja nchini kwetu walikuwa wakipata shauku ya kutamani kukumbana na huduma yake ya kipekee ya Mzee huyu mwenye upofu wa macho.
Mzee huyu ambaye kwa sasa ameshafariki tayari, alikuwa ni tunu ya Taifa kwenye sanaa. Ni miaka mingi imepita hakumbukwi popote hata pengine kwenye vyuo vyetu vya sanaa.
JE WEWE MPENDWA UNAMZUNGUMZIAJE MZEE WETU HUYU?
HUYU NDIYE MZEE MORRIS NYUNYUSA KIPOFU MPIGA NGOMA WA TANGU ZAMANI.
Reviewed by Erasto Paul
on
August 03, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili