Wakati
matokeo ya mitihani ya kidato cha sita yakitolewa leo, Jumamosi Julai
15, imebainika kuwa watahiniwa 10 walifutiwa matokeo kwa makosa ya
kufanya udanganyifu.
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta),
Dk Charles Msonde imeeleza kuwa kati ya watahiniwa hao kumi, saba ni wa
shule na watatu ni wa kujitegemea.
Pamoja na hao kumi, matokeo ya watahiniwa wengine 15 yalizuiliwa kwa kuwa hawakufanya mitihani ya baadhi ya masomo.
Watahiniwa
hao walishindwa kufanya mitihani kutokana na matatizo mbalimbali
ikiwamo ya kiafya na hivyo kushindwa kufanya baadhi ya mitihani hiyo.
‘Watahiniwa
hao wamepewa fursa ya kufanya mitihani ya kidato cha sita, Mei 2018
kama wa watahiniwa wa shule,” imesema taarifa ya Dk Msonde.
Pia,
wapo watahiniwa 69 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na
kushindwa kufanya mitihani yote, wamepewa fursa ya kufanya mitihani
hiyo, Mei 2018.
Wanafunzi 10 Wafutiwa Matokeo Kidato cha Sita
Reviewed by Erasto Paul
on
July 15, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili