Uhakika, Rooney Athibitisha Kutua Bongo

https://globalpublishers.co.tz/wp-content/uploads/2017/07/Rooney-tZ.jpg
Uhakika ni kuwa staa wa soka wa England, Wayne Rooney anatarajiwa kutua nchini Tanzania akiwa na kikosi chake cha Everton kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.

Everton inatarajiwa kucheza mchezo huo ikiwa ni maandalizi kujiandaa na msimu ujao wa 2017/18, ambapo timu hizo zinakutana chini ya udhamini wa SportPesa ambao ndiyo wadhamini wa kuu wa Everton.

Kampuni ya SportPesa iliandaa michuano ya SportPesa Super Cup iliyofanyika jijini Dar es Salaam na Gor Mahia kuwa bingwa ambapo ndipo watakutana na Everton ili kukamilisha michuano hiyo ya mwaka huu, mchezo utachezwa kwenye Uwanja wa Taifa.

Rooney mwenyewe amesema safari hiyo itamsaidia kujuana vizuri na wachezaji wenzake.
Mchezaji huyo ambaye anaongoza kwa mabao ya kufunga katika timu ya taifa ya England amerejea kwenye kikosi cha Everton baada ya kuondoka miaka 13 iliyopita.

Nahodha huyo wa zamani wa Manchester United, ameshaanza mazoezi ya pamoja na wenzake, atakuwemo kwenye msafara huo chini ya Kocha Ronald Koeman.

Akiwa Everton, Rooney, 31 atakutana na Morgan Schneiderlin pamoja na Michael Keane ambao alicheza nao pamoja Manchester United, wakati Phil Jagielka, Leighton Baines na Ross Barkley amekuwa akikutana nao kwenye majukumu ya timu ya taifa.

“Naisubiri kwa hamu, naamini itakuwa safari nzuri, tutapata nafasi ya kucheza na kujuana, ni jambo zuri unaposafiri na timu, kuwa hoteli moja, kuwa pamoja muda mwingi, hiyo itasaidia kujuana vizuri.
“Sijawahi kufika Tanzania kabla naamini nitafurahia safari yangu,” amesema Rooney.
Uhakika, Rooney Athibitisha Kutua Bongo Uhakika, Rooney Athibitisha Kutua Bongo Reviewed by Erasto Paul on July 10, 2017 Rating: 5

No comments:

Thank you for commenting to Mwanauswahili

Powered by Blogger.