Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limeifungia shule ya sekondari ya Alliance Girls ya Mwanza kuwa kituo cha mitihani kutokana na ukiukwaji wa kanuni za mitihani ikiwemo udanganyifu.
NECTA imeagiza kamati ya uendeshaji wa mitihani ya mkoani Mwanza kuwatafutia watahiniwa wa shule hiyo kituo kingine cha kufanyia mitihani.
Akizungumzia udanganyifu uliobainika kwenye shule hiyo, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt. Charles Msonde amesema wakati wa mtihani wa Biology 1, mtahiniwa S4836/0502 wa shule hiyo alikamatwa akiwa na karatasi yenye ‘notes’, ambayo baada ya kukamatwa iliunganishwa na maelezo ya mashahidi, maelezo ya mtahiniwa kukiri kosa na karatasi ya kujibia mtihani ya mtahiniwa ambapo vyote viliwekwa kwenye bahasha.
Dkt. Msonde ambaye alikuwa akitangaza rasmi matokeo ya kidato cha sita
kwa mwaka 2017, amesema katika hali ya kushangaza, bahasha husika
ilipofunguliwa wakati wa usahihishaji, ilibainika kuwa vielelezeo vyote
vilikuwa vimeondolewa.
Msonde ameendelea kusema baada ya uchunguzi kufanyika, ilibainika kuwa wasimamizi wa mtihani na askari aliyekuwa analinda kituo hicho walifungua bahasha na kuondoa vielelezo vyote na kisha kuifunga upya bahasha ile.
Amesema uchunguzi zaidi ulibaini kuwa mmiliki wa shule hiyo pamoja na mwalimu mkuu walihusika katika tukio hilo, hivyo kutokana na shule hiyo kupewa onyo mara kadhaa, Baraza hilo limeaua kutumia mamlaka yake kukifungia hadi litakapoamua vinginevyo.
Azam Tv.

NECTA YAIFUNGIA SHULE YA ALLIANCE GIRLS'
Reviewed by Erasto Paul
on
July 15, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili