Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema ameridhishwa na maendeleo ya mradi wa kufua
umeme wa Kinyerezi II ambao ukikamilika utazalisha jumla ya megawati 240
zitakazoingizwa kwenye gridi ya Taifa.
Majaliwa
ametoa kauli hiyo leo Jumamosi, baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya
ujenzi wa mradi huo uliopo eneo la Kinyerezi katika Manispaa ya Ilala
jijini Dar es Salaam.
Amesema
baada ya kukagua amejionea kazi nzuri inayoendelea katika ujenzi wa mradi huo
unao tekelezwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Sumitomo ya
Japan.
"Mradi
huu ni wa kimakakati kwa ajili ya kuzalisha umeme ili Watanzania wapate nishati
hii kwa bei nafuu. Ndiyo Maana Serikali imeamua kuanzisha uhusiano na balozi
tofauti kwa ajiki ya kutekeleza miradi mbalimbali," amesema Majaliwa.
Amesema
lengo la Serikali ni kuhakisha nishati ya umeme inafika vijijini kupitia mradi
unaotekelezwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) ambao umeonekana kufanya vizuri
katika maeneo mengi nchini.
Alilitaka
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuendelea kusambaza umeme kwa wananchi
wengi.
Majaliwa aridhishwa na mradi mkubwa wa umeme
Reviewed by Erasto Paul
on
July 08, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili