Maafisa wa polisi nchini Uganda
wamemkatama msomi mmoja ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa familia ya
rais Museveni katika taifa hilo la Afrika Mshariki.
Nyanzi atashtakiwa siku ya Jumatatu kwa makosa hayo kwa kutumia tarakalishi kunyanyasa mbali na kuandika maneno ya kukera.
Nyanzi ni maarufu katika mtandao wa facebook kwa ukosoaji wa rais Yoweri Museveni ambaye ameliongoza taifa hilo tangu 1986.
Wakosoaji wa Museveni wanaonya kuwa rais huyo anataka kuliongoza taifa hilo kwa maisha.
Baadhi ya mawakili wa Uganda wamekuwa wakisema wataunga mkono pendekezo la kuondoa kiwango cha umri katika katiba hatua ambayo huenda ikawa ya mwisho ya uongoza wa maisha wa rais Museveni.
Katika ukurasa wake wa facebook Nyanzi alimkemea mke wa rais, Janet Museveni ambaye ni waziri wa elimu kwa kusema serikali haina fedha za kununua sodo kwa wasichana masikini wa shule licha ya rais aliahidi kuwahifadhia fedha wakati alipkuwa akifanya kampeni za uchaguzi mwaka uliopita.
Wasichana wengi nchini Uganda wameripotiwa kuacha masomo kutokana na aibu ya kukosa sodo.
''Ninakataa wazo kwamba mtu hawezi na hafai kukosoa watu wanaonyanyasa haki na mali za Waganda katika miaka 31 ya uongozi wa kidikteta wa familia moja'', alisema katika chapisho moja la facebook.
''Kama mtu anayefikiri, msomi, mshairi, mwandishi mmiliki wa akaunti ya facebook na mtayarishaji ni jukumu langu kuwakosoa wafisadi wa siku hizi''.
Nyanzi alimtaja mke wa rais kuwa 'mjinga' na asiyejua maswala yanayowaathiri Waganda.
Msomi huyo ambaye ni mwanaanthropolojia hutumia picha za ngono kupitisha ujumbe wake.
Lakini mashabiki wake wanasema yeye ni mwanaharakati mwaaminifu ambaye hutumia ujuzi wake wa fasihi kupigania maskini.
Mwanaharakati akamatwa kwa 'kumtusi' Janet Museveni
Reviewed by Erasto Paul
on
April 10, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili