Zipo njia nyingi ambazo zimetajwa kuwa zinaweza kumfanya mtu adumishe afya yake kwa ujumla wake ambazo ni pamoja na kuzingatia kanuni za afya, kudumisha usafi, kula aina za vyakula vinavyoshauriwa na wataalamu wa afya na kuishi katika mazingira salama.
Leo nimekutana na hii ya aina sita za virutubisho kwa ajili ya afya bora na kuinua kinga za mwili
1: Omega-3 Fatty Acids ambayo hupatikana kwenye mafuta ya samaki yana faida kubwa kwa afya na mfumo wa kinga
Mwili wa binadamu hauwezi kutengeneza acid ya omega-3 fatty hivyo binadamu anahitaji kuipata kwenye chakula au virutubisho hasa mafuta ya samaki ambayo husaidia mfumo wa kinga za mwili kwa kupunguza uvimbe na kuimarisha blood chemistry.
Mafuta ya samaki huimarisha afya ya ubongo na afya ya moyo, kwa kutoa ulinzi dhidi ya saratani, huzuni, matatizo ya utumbo, na yabisi.
2: Madini ya magnesium
Zaidi ya nusu ya madini ya magnesium kwenye mwili ni kwa ajili ya kuimarisha mifupa. Wakati calcium ikikaza misuli, magnesium hufanya kinyume chake kwa kuilegeza. Ingawa magnesium ni muhimu kwa afya ya mifupa pia hufanya kazi nyingi sana mwilini.
3: Probiotics ambayo husaidia kujenga kinga asili za mwili dhidi ya magonjwa mengi na kinga kwa ajili ya mzio ‘allergies’
Kuwa na mfumo wa kinga wenye afya, mfumo wa utumbo unatakiwa uwe na uwiano sawa wa bacteria sahihi kwa kiwango sahihi.
Bacteria hawa huukinga mwili kutokana na vikwazo mbalimbali.
Bacteria wasipokuwa kwa kiwango sawa, inaweza kutokea gut dysbiosis ambayo hufungua milango kwa matatizo ya autoimmune, saratani, kisukari na matatizo ya ngozi.
4: Vitamin C ni mponyaji mzuri
Vitamin C husaidia kuzuia mafua na homa kutokana na uwezo wake wa haraka katika kuchochea uzalishaji wa cell mpya kwenye kuponya kidonda hivyo kuukinga mfumo wa kinga za mwili na kusaidia kupambana na maambukizi.
Mwili wa binadamu hauwezi kutengeneza vitamin C hivyo unalazimika kuzipata kupitia diet au virutubisho ambapo baadhi ya vyanzo vya asili vya Vitamin C ni pamoja na machungwa na mboga za kijani.
5: Uwiano sawa wa Vitamin D3
Hii huweza kukuepusha na magonjwa mengi kama vile saratani na mafua ambapo vitamin D3 ni mlinzi wa kinga huku pia ikiwa ni muhimu kwa afya ya mifupa. Unashauriwa ili kusawazisha vitamin D3 unatakiwa kuchagua nyama na mayai katika mlo wako.
6: Zinc hupunguza muda na makali ya dalili za mafua
Kama akiba yako ya zinc iko sawa huhitaji virutubisho, lakini kama haiku sawa virutubisho vitakusaidia kuepuka mafua. Kama unakula vyakula kama kiini cha yai, mbegu za alizeti, mbegu za maboga utakuwa na afya nzuri.
Hizi Hapa Aina sita za virutubisho ambavyo unaambiwa vinainua kinga za mwili
Reviewed by Erasto Paul
on
March 30, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili