Kufuatia
malalamiko yaliyotolewa na mwenyekiti wa mtaa wa buguruni Mjini Njombe Emanuel
Ngelime kuhusu kupigwa vibao mkuu wa
wilaya ya Njombe bi Ruth Msafiri ,Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Jimbo la Njombe kimetangaza rasmi kutokufanya
kazi na mkuu huyo kuanzia sasa.
Tamko
hilo linaambatana na kumtaka mkuu huyo kumuomba radhi mwenyekiti huyo ambaye
anahudumu katika serikali ya mtaa kwa tiketi ya chadema ndani ya siku saba
kuanzia leo march 7,2017.
Chama
hicho kinasema kamwe hakiwezi kufanya kazi na kiongozi ambaye anatumia nafasi
yake tofauti na sheria ikiwemo nguvu za mabavu na lugha za kejeli kwa wenyeviti
wa serikali za mitaa.
Mwenyekiti
wa chadema wilaya ya Njombe Abuu Mtamike amesema jambo hilo halivumiliki anachotakiwa
ni kuomba radhi ili kuendelea kuaminiwa na wananchi anaowaongoza.
Mtamike
ameongeza kuwa kinachoonekana mkuu huyo
anafanya kazi ya siasa na kuacha majukumu yake na kwamba nia ya mkuu huyo ni
kudhoofisha vyama vya upinzani mjini Njombe na hasa Chadema.
Kwa
Upande wake Mwenyekiti wa madiwani wa chadema jimbo la Njombe Mjini George
Sanga kwa nafasi yake anasema pia kama madiwani nao hawako tayari kutoa
ushirkiano wowote kwa mkuu huyo hadi
pale aatakapo omba radhi ka kitendo alichofanya.
Naye
mwenyekiti wa wenyeviti wa serikali za mitaa zinazoongozwa na chadema Brayson Nickodemas
Mgaya anasema mara kadhaa mkuu huyo wa wilaya amekuwa akitembelea katika mitaa
mbalimbali na kufanya shughuli za ukaguzi wa miradi na hasa mashuleni bila
kuwashirikisha wenyeviti wa mitaa husika.
February
28 mwaka huu Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Ruth Msafiri alidaiwa kimtandika makofi Mwenyekiti wa Mtaa
wa Buguruni –Matalawe Emmanuel Ngelime
mara baada ya kutokuwepo kwa maelewano baina ya viongozi hao wawili.
Hata hivyo Siku Moja Baadaye Mkuu huyo wa Wilaya alikanusha taarifa za kuhusika kumtandika vibao mwenyekiti huyo jambo lililoongeza Gumzo kwa wanachi hususani wananchama wa CHADEMA.
CHADEMA NJOMBE KUTOFANYA KAZI NA DC ALIYEMTANDIKA MAKOFI MWENYEKITI WA MTAA.
Reviewed by Erasto Paul
on
March 07, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili