Habari ndugu msomaji wa blog ya Kilimo Biashara, ni matumaini yangu unaendelea vizuri na mapambano ya kuelekea kwenye mafanikio kupitia kilimo. Karibu tena katika kona hii ya kupata maarifa ya kilimo.
Kutokana na maombi na maswali kadhaa ya watu kuhusu Kilimo cha Greenhouse, leo nitapenda tuanze kujifunza kuhusu mada hiyo ya Greenhouse.
Leo tutaangazia kwanza maana ya teknolojia hiyo, historia yake, faida zake, Aina zake, pamoja na matumizi na mapato kwa baadhi ya Greenhouse
Karibu sana:
Kwanza tuanze kwa kupata tafsiri ya neno lenyewe, Greenhouse imekua ikipatiwa majina tofauti tofauti, wapo watu wanaiita Nyumba ya Kijani, wengine wanaiita Banda Kitalu n.k Vyovyote utakavyopenda kuiita teknolojia hii, cha muhimu ni kuelewa nini hasa maana yake.
Greenhouse(Banda Kitalu): ni
teknolojia ya kuipatia mimea mazingira mazuri ambayo yataisaidia
mimea/mazao kumea vizuri na kua na uzao mkubwa, mimea hii inapandwa
kwenye banda, au nyumba maalumu. Teknolojia hii inatumika hasa kuikinga
mimea usiathiriwe na mazingira haribifu ya hali ya hewa. Mazingira
haribifu ni kama upepo mkali, baridi kali, mvua kubwa, au mvua za mawe,
mionzi mikali ya jua, joto kali , wadudu pamoja na magonjwa. Hayo ndio
mazingira ambayo teknolojia hii inaleta suluhisho, kuhakikisha mimea
inastawi vizuri bila ya kuathiriwa na moja ya matatizo hayo yaliyotajwa.
Teknolojia
hii ilivumbuliwa huko kwenye nchi baridi, zaidi ya karne moja na nusu
(miaka 150) iliyopita. Nchi zilizopo ukanda wa baridi, mazao ya
kitropiki (mazao yanayo pendelea joto) ilikua haiwezekani kabisa kulimwa
maeneo hayo ya ukanda wa baridi. Ndipo hapo wazo la kuvumbua Greenhouse
lilipoibuka. Nchi hizi walianza kutumia teknolojia hii maana nyumba hii
ya kijani ilikua ina uwezo wa kutunza joto, na hivyo wakaanza kulima
mazao ya ukanda wa joto kama mbogamboga (nyanya, hoho) na matunda.
Pamoja na teknolojia hii kuanza kitambo kidogo katika nchi
zilizoendelea, lakini kwa upande wa nchi zinazoendelea bado teknolojia
hii ni mpya kwa watu wengi. Teknolojia hii pia inatumika katika nchi za
joto, japo kuna utofauti kati yake na zile za nchi za ukanda wa
baridi.
Faida za Greenhouse
- Mavuno yanakua mara 10 hadi 12 zaidi ya kilimo cha eneo la wazi, ikitegemea aina ya mazao yanayolimwa humo, aina greenhouse pamoja na vifaa vya kudhibiti mazingira ya ndani ya greenhouse.
- Uhakika wa kuvuna mazao unaongezeka. Maana Greenhouse inaweza kuzuia visababishi vya uharibifu wa mazao.
- Uzalishaji wa mazao katika kipindi chote cha mwaka, maana huhitaji kusubiri mpaka msimu wa zao ufike ndio ulime.
- Uwezo wa kupata soko zuri la mazao. Greenhouse itakuwezesha kuzalisha kipindi ambacho sio cha msimu (off- season) kwa vile kipindi hiki watu wengi hawazalishi kutokana na mazingira kutoruhusu, ukiwa na greenhouse una uwezo wa kuzalisha kipindi hicho na ukapata bei nzuri
- Ufanisi katika utumaji wa dawa, viwatilifu katika kudhibiti.
- Matumizi ya maji ni madogo sana na udhibiti wake ni rahisi. Miundombinu ya umwagiliaji inayotumika hapa ni umwagiliaji wa matone (drip irrigation) ambapo maji yanakwenda pale penye mmea pekee.
- Uwezo wa kutunza mimea inayozalishwa maabara kutokana na teknolojia ya tishu (tissue culture technology) mimea inapotoka maabara kabla haijapelekwa shambani inatunzwa kwanza kwenye greenhouse maalumu kwa ajili ya kuzoea mazingira ya nje kwanza.
- Uwezo wa kupanda mimea bila kutumia udongo (soilless culture). Kutokana na changamoto ya magonjwa na vijidudu vya kwenye udongo kama Nematodes, ndipo uvumbuzi wa teknolojia ya kupanda mimea kwa kutokutumia udongo ulipotokea
Baadhi ya Nchi zinazofanya vizuri kilimo cha Greenhouse.
- Kuna nchi zaidi ya 50 katika dunia ambapo kilimo kinalimwa kwenye greenhouse. Tutaangalia baadhi ya nchi ambazo zimekua zikifanya vizuri kupitia teknolojia hii. Tuanze na Marekani, Marekani ina eneo takribani 4000 hekta ambazo zina greenhouse kwa ajili ya kilimo cha maua, Marekani kupitia kilimo hicho wanapata pato la zaidi ya Dola bilioni 2.8 (zaidi ya trilioni 5 hela za Tz) kwa mwaka. Nchini Hispania inakadiriwa zaidi 25,000hekta na Italia ni hekta 18,500, zimefungwa greenhouse kwa kilimo cha pilipili hoho, strawberry, matango, maharagwe machanga, pamoja na nyanya.
- Canada greenhouse ni kwa kilimo cha maua na mboga mboga wakati ambapo hazilimwi kwingine. Mazao maarufu yanayolimwa kwenye Greenhouse za Canada kama nyanya, matango na hoho.
- Uholanzi ni zaidi ya hecta 89,600 zipo nchini ya greenhouse. Uholanzi sekta ya greenhouse ndio iliyo bora zaidi duniani. Uholanzi ndio nchi inayoongoza kwa teknolojia hii na wamepiga hatua mbali sana. Yapo makampuni makubwa ya Kiholanzi yanayotumia teknolojia hii baadhi yao yapo hapa Tanzania katika kilimo cha maua, matunda, mbogamboga, pamoja na mbegu. Mfano : Kili Hortex, Multi flower, Mount Meru Flower, Enza Zaden, RJK ZWAAN (Q-SEM na AFRISEM)
- Israel: 15000 hekta. Israel ndiyo nchi inayoongoza kwa kuuza maua (cut flowers) nje ya nchi. Japokuwa nchi ya Israel eneo lake kubwa ni jangwa. Pia Nchi ya Israel imekua moja ya nchi zilizopo mstari wa mbele katika teknolojia ya umwagiliaji na Greenhouse. Balton Tanzania yenye makao yake makuu mjini Arusha, ni moja ya kampuni toka Israel zinazofanya vizuri katika sekta hii.
- Uturuki: hekta 10,000 zinalimwa maua na mbogamboga kwa kutumia teknolojia hii ya Green house. Saudi Arabia: 90% ya mazao ya yanya na tango yanalimwa kwenye green house.
- Misri 10,000 hekta nyanya, matango na pilipili hoho. Teknolojia ya Greenhouse nchini China inakua kwa kasi sana kuliko nchi yeyote Japokuwa teknolojia hii haijaanza muda mrefu kivile huko China lakini mpaka sasa zaidi ya hekta 48,000 tayari zimefungwa Greenhouse. Nchi nyingine zinzofanya vizuri barani Asia ni kama Japan (40,000hekta) na Korea kusini (21,000 hekta).
Aina za Greenhouse.
Greenhouse zinagawanyika makundi mbalimbali kutegemeana na vigezo vifuatavyo:
- Aina za Greenhouse kwa kigezo cha sura/umbile (shape)
Zipo aina aina 8 za greenhouse, hapa nitataja chache tu kwa majina yake ya kitaalamu
- Quonset Greenhouse
- Saw tooth type
- Even span type greenhouse
- Uneven span type greenhouse
- Aina za Greenhouse kwa kigezo cha Matumizi
- Green house zinazoongeza joto (Hizi ni kwa maeneo ya baridi)
- Greenhouse zinazopunguza joto (hizi ni kwa maeneo ya joto)
- Aina za greenhouse kwa kigezo cha matengenezo yake (construction)
- Greenhouse za miti (Wooden framed structure)
- Pipe framed structure (Greenhouse zinazotumia mabomba)
- Truss/Aluminium framed structure ( Geenhouse zinazojengwa kwa vyuma)
- Aina za Greenhouse kwa kigezo cha aina ya zana za ufunikaji (covering types)
- Greenhouse zinazofunikwa kwa zana za Vioo (Glass Greenhouse or Screenhouse) )- hizi zinatumika sana maeneo ya baridi kali, ili kutunza joto kwa muda mrefu ndani greenhouse
- Greenhouse zinazofunikwa kwa mifuko ya plaski (plastic film)
- Aina ya Greenhouse kwa kigezo cha uwekezaji unaofanywa:
- Greenhouse za gharama kubwa (High cost greenhouse) ( Zaidi ya milioni 50)
- Greenhouse za gharama za kati (medium cost greenhouse) (milioni 20 hadi 50)
- Greenhouse za gharama ndogo (Low cost greenhouse) (chini ya milioni 20)
Greenhouse za gharama ndogo ndio watu wengi wanazitumia sana katika nchi
zinazoendelea. Hapa chini tumeweka mapato na matumizi ya baadhi ya
Greenhouse za bei nafuu.
Kwa wanaohitaji greenhouse Na Net house, bei zake ni kama ifuatavyo:
GREENHOUSE
I. 6m * 12m - Milioni 3.5
II. 8m*15m. - Milioni 5.5
III. 8m*30m - Milioni 10.5
IV. 16m*30m -Milioni 15
NET HOUSE – Hii inafaa sana kwa yale maeneo ya joto.
I. 6m * 12m- Milioni 3
II. 8m*15m - Milioni 4
III. 8m *30m- Milioni 9
IV. 16m * 30m - Milioni 12
NB: Tutakufungia Ukubwa wowote unaotaka
Package inakuwa Na:
- Utapewa Elimu Kwanza ya Kutosha Greenhouse/ Net House na Drip Irrigation
-Kujengewa greenhouse / Net house Kwa kutumia Miti Imara ya Miti, inayodumu Kwa Miaka kuanzia 15.
- Kufungiwa vifaa vya umwagiliaji matone( drip irrigation)
- Kufungiwa tank la Maji kuanzia lita 1000, 2000 n.k kutokana na ukubwa wa Greenhouse/Net house
- Kupewa mbegu ya zao unalohitaji na yenye kutoa mazao mengi
- Tray za kupandia
- Udongo Maalum wa Kupandia
- Kufungiwa crop support
- Kupandiwa
-Unakabidhiwa greenhouse/Net House ,ikiwa imekamilika na kwa kila kitu
- Kutembelewa na Kupewa
- Kupima Udongo
-Ushauri wa Kitaaalam ili utoe mazao Organic
- Tutakusaidia kuhifadhi
kitaalam, kwenye kontena Maalum Kwa ajili ya kusafirisha kupeleka sokoni.
- Kusaidiwa kutafuta Soko la Ndani Na Nje ya Nchi.
Nyongeza
-Tunatumia Materials kutoka ISRAEL, Na tuna wataalam waliobobea katika
ujenzi wa greenhouse /net house Kwa muda mrefu pia wataalam wa kilimo.
-Tutakufuata popote pale ulipo Tanzania Tanzania
-Utapewa Elimu ya Kutosha kuhusu Greenhouse/Net house na Faida kubwa utakayopata ndani ya Mwaka Mmoja
+ Pia tunafunga Drip irrigation kwenye Shamba lolote la wazi
Pia tunazo Green house za chuma (Metal) toka Israel. Hizi zinadumu kwa muda mrefu sana.
- Ni Greenhouse imara sana, una uwezo wa kubeba uzito wa 35kg kwa mita moja ya mraba (35Kg per square meter).
- Zinakuja na crop support cables kwa ajili ya mazao kama Hoho, nyanya na matango
Bei za Greenhouse za Chuma ni kama Ifuatavyo:
10*12 M = USD 3,000 (TZS: 6,700,000)
10*24 M = USD 5,000 (TZS: 11,165,000)
Kwa Mawasiliano
Piga: 0763 071007
email: ushauri@kilimobiashara.net
FURSA KUPITIA TEKNOLOJIA YA KILIMO CHA GREENHOUSE
Reviewed by Erasto Paul
on
February 22, 2017
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili