Baadhi ya wazee wanaopatikana katika halamashauri ya wilaya ya Wanging’ombe Leo wanatarajia kufanya maombi ya jadi kadri ya mila zao ili kuishinikiza mvua iweze kunyesha kama ilivyozoeleka katika mikaa iliyopita.
Maombi hayo yatafanyika kukiwa bado kuna hali ya sintofahamu pamoja na kuwepo ukame uliokithiri miongoni mwa maeneo hususani ya wakulima waliopo mkoni Njombe na mikoa ya Jirani.
Kitendo cha mvua kunyesha kwa kusuasua na maeneo mengine kutonyesha kabisa kwa mwaka huu kimewapiga Bumbuwazi wananchi wa mkoa wa Njombe kiasi cha kubaki Njia Panda wasijue la kufanya.
Katika maombi hayo akina Bibi waliobobea katika maswala ya mila na desturi ndiyo viongozi wa maombi hayo ya utekelezaji mila ambayo yanatajwa kuwa yanaweza kusaidia watu kujiokoa na janga la Njaa.
Taaasisi za Kidini Nchini zimetakiwa kuungana na wazee hao kwenye maombi ili kuliombea taifa na watanznaia kwa ujumla.
WAZEE WANGING'OMBE KUFANYA TAMBIKO LA JADI ILI KULETA MVUA
Reviewed by Erasto Paul
on
December 28, 2016
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili