Tetesi; T.I. na mkewe huenda wasipeane talaka.

Tiny anaweza akawa ameomba talaka kutoka kwa mumewe T.I., lakini kwa mujibu wa TMZ, huenda huo ukawa sio mwisho wa ndoa hiyo.

Tovuti hiyo imedai kuwa kuna dalili za wanandoa hao kusuluhisha matatizo yao na kuendelea kuwa pamoja ni kubwa.

Ripoti mpya imedai kuwa wawili hao wamekuwa kwenye maelewano mazuri tangu Tiny adai talaka yake, Dec. 7 na wamekuwa pamoja kwa ukaribu zaidi, kwa mujibu wa vyanzo. Wamedaiwa pia kusherehekea sikukuu ya Christmas pamoja na familia yao.

Wamekuwa pamoja kwa miaka 20 lakini walifunga ndoa rasmi mwaka 2010 na hadi sasa wana watoto watatu pamoja, King, Major, na Heiress Harris huku T.I. akiwa na watoto wengine wa nje ya ndoa, Messiah, Domani, na Deyjah Harris na Tiny ana binti aliyemzaa kwenye uhusiano uliopita, Zonnique Pullins.
Tetesi; T.I. na mkewe huenda wasipeane talaka. Tetesi; T.I. na mkewe huenda wasipeane talaka. Reviewed by Erasto Paul on December 29, 2016 Rating: 5

No comments:

Thank you for commenting to Mwanauswahili

Powered by Blogger.