Haya ndio majibu ya Mourinho ya kumchezesha Fellaini

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho ametetea uamuzi wake wa kumuingiza uwanjani kiungo wa kati Marouane Fellaini kama nguvu mpya wakati wa mechi ambayo walitoka sare na Everton Jumapili.
http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2016/12/92826782_jose_mourinho_fellaini_getty.jpg
Fellaini baada tu ya muda mfupi kuingia alisababisha penalti dakika ya 85, na kuwawezesha Everton kusawazisha na mambo yakawa 1-1.

Alipoulizwa kuhusu uamuzi wake, Mourinho alisema alimwingiza kwa sababu ya kimo chake na uchezaji wa Everton.

“Nilifikiri kwamba mnafaa kuwa mnajua mengi zaidi kuhusu soka kuliko mlivyo,” Mourinho alisiema akiongea na wanahabari.

“Everton si timu ya kutoa pasi kama walivyokuwa zamani. Everton ya sasa ni klabu inayocheza moja kwa moja: kipa moja kwa moja, Ashley Williams moja kwa moja, Ramiro Funes Mori moja kwa moja. Kila kitu moja kwa moja.

“Unapokuwa na mchezaji wa kimo cha mita mbili kwenye benchi unamchezesha kwenye safu ya ulinzi kuisaidia timu kushinda mipira.”
Haya ndio majibu ya Mourinho ya kumchezesha Fellaini  Haya ndio majibu ya Mourinho ya kumchezesha Fellaini Reviewed by Erasto Paul on December 05, 2016 Rating: 5

No comments:

Thank you for commenting to Mwanauswahili

Powered by Blogger.