Bondia
maarufu nchini Tanzania Francis Cheka, jana ametangaza rasmi kustaafu
mchezo wa msumbwi kwa kile alichokieleza ni ubabaishaji wa ma-promota
pamoja na kutopata faida katika mchezo huo.
Cheka
ambaye anakabiliwa na tuhuma za kuchukua pesa na kugoma kupanda
ulingoni katika pambano lililokuwa limeandaliwa siku ya Krismasi,
amesema amechoshwa na kile alichokiita kuwa ni utapeli wa mapromota, na
kwamba sasa atajikita zaidi katika mapambano ya kuhamasisha vijana.
Akiwa
amedumu kwenye ngumi nchini kwa takribani miaka 19, Cheka amesema
mchezo huo umetawaliwa na majungu, na fitina huku watu wengi wakifikiri
kuwa kuna pesa nyingi, wakati hakuna anachokipata zaidi ya umaarufu na
kuhojiwa kwenye vyombo vya habari.
"Huu
mchezo una majungu na fitina, hakuna faida yoyote zaidi ya kuhojiwa na
waandishi wa habari, hakuna pesa, tunapata pesa gani, watu wanadhani
tunapata pesa, nitabaki kucheza mapambano kwa ajili ya kuhamasisha
vijana katika ngumi pamoja na kufanya biashara nyingine nipate pesa,
nimedumu kwenye ngumi zaidi ya miaka 19, nimevumilia mengi" Alisema Cheka.
Francis Cheka atangaza ramsi kustaafu ngumi
Reviewed by Erasto Paul
on
December 30, 2016
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili