
Wiki
moja baada kutokea ajali mbaya ya ndege iliyokuwa na wachezaji wa timu
ya Chapecoense inayoshiriki Ligi Kuu ya Brazil na kuua abiria 71
wakiwemo wachezaji wa timu hiyo, waandishi wa habari, makocha na
wafanyakazi wa ndege hiyo, imetoka ripoti kuwa mchezaji Helio Neto
aliyenusurika alikuwa akisoma Biblia kabla ya kutokea ajali.


Kwenye
kipande kifupi cha Video kilichoonekana kwenye camera za ndege hiyo
kimeonesha kuwa mchezaji huyo alikuwa akisoma Biblia muda mwingi akiwa
kwenye ndege na hata baada ya ajali bado Biblia ilikutwa kwenye siti
yake pamoja na yeye Neto kuwa kwenye hali mbaya.
Ukurasa ulioonekana kwenye Bibla ilikuwa ni kutoka kwenye kitabu cha Zaburi 63:6-8. Ambayo ina maneno haya;
“Wakati
ninapokukumbuka kitandani mwangu, wakati wa makesha ya usiku natafakari
juu yako. Kwa maana umenisaidia na katika kivuli cha mabawa yako napiga
vigelegele kwa shangwe, nafsi yangu imekufuata karibu, mkono wako wa
kuume unanishika sana.”

Jumla ya
watu 71 walipoteza maisha kwenye ajali ya ndege aina ya Avro RJ85
iliyotengenezwa nchini Uingereza baada ya kuanguka kwenye milima
ya Medellin nchini Colombia, ambako timu ya Chapecoense ilikuwa inaenda
kucheza fainali za Copa Sudamericana.
Source;millardayo.com
Biblia ilivyookoa maisha ya mchezaji wa Chapecoense “Neto” kwenye ajali ya Ndege
Reviewed by Erasto Paul
on
December 09, 2016
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili