Kifupi, Wema baada ya kuchukua Taji la Miss Tanzania Mwaka 2006 akiwa bado hajafikisha umri wa miaka 18, amefanikiwa kuliweka jina lake juu katika kipindi chote hicho, kufuatia tabia zake nje ya sanaa ya urembo, lakini pia akionyesha kipaji cha hali ya juu kwenye filamu, mara tu baada ya kuingizwa mchezoni na hayati Steven Kanumba.
Kwa hakika kabisa, Wema ni mmoja kati ya waigizaji wachache wenye kipaji cha ukweli cha uigizaji, ingawa mara nyingi amekuwa akiangushwa na mfumo wa utengenezaji wa filamu za Kibongo, ambazo zimekuwa za kuigana na zinazotoka nje ya mstari zinapooanishwa na uhalisia.
Anajua nini anapaswa kufanya katika eneo lake na unaweza kunielewa vizuri zaidi kama utazitazama filamu kadhaa alizocheza kama The Point of no Return na Red Valentine, kwa sababu anapotakiwa kuwa mnyenyekevu, anakuwa, anapotakiwa kuwa anayenyanyaswa anakuwa, kitu ambacho kinawashinda wengi.
Huenda hii ni moja ya sababu inayomfanya binti huyo kuwa na mashabiki wengi pengine kuliko waigizaji wote wa kike nchini. Ni msanii anayeweza kujaza ukumbi kwa shughuli zake zinazowaingiza mashabiki wengi na amethibitisha hivyo katika maeneo mengi alikoandaa matukio, Dar, Mwanza, Arusha na kwingineko Tanzania.
Wem
Sepetu ‘Madam’ akidendeka na mwanaume mwenye asili ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakiwa kwenye Mgahawa wa hoteli iliyopo
Msasani jijini Dar mwaka jana.
Ingawa kila mmoja anapaswa kuheshimiwa kutokana na aina ya maisha aliyoamua kuishi, lakini pia hadhi na umaarufu wa mtu, humlazimisha kuishi aina f’lani ya maisha hata kama hapendi.
Kwa mfano, mtu mwenye hulka ya kujirusha
viwanja hawezi kuendelea kuwa wa hivyo endapo atafanikiwa kuwa rais wa
nchi. Hadhi yake itamzuia kuzurura na kuonekana maeneo ya namna hiyo kwa
nyakati hizo.
Hivyo ndivyo pia wanavyotakiwa kuwa watu wanaojipatia umaarufu katika jamii kutokana na jinsi wanavyofanya sanaa zao, michezo au fani yoyote yenye kufuatiliwa kwa ukaribu na mashabiki.
Unapomzungumzia Wema Sepetu, ni kama unaongelea aina ya mtu ambaye
mwili wake unakosa heshima inayostahili. Ingawa waigizaji wengi wa
Kibongo wanatajwa kama wenye tabia zisizopendeza, lakini kwa huyu Madam
ni kiboko!Hivyo ndivyo pia wanavyotakiwa kuwa watu wanaojipatia umaarufu katika jamii kutokana na jinsi wanavyofanya sanaa zao, michezo au fani yoyote yenye kufuatiliwa kwa ukaribu na mashabiki.
Ana orodha ndefu ya wanaume wanaotajwa kutoka nao. Mr Blue, TID, Steven Kanumba, Chaz Baba, Jumbe, Diamond na Idris Sultan ni miongoni mwao, ukiachilia mbali madai ya kujirusha na kigogo wa ikulu, Wakongo na majina mengine mengi mengi!
Huenda labda ni kwa vile Wema Sepetu ni bonge la mtoto? Au inawezekana huyu binti ni maharage ya Mbeya? Sijui, huenda pia kama wanavyosemaga kuwa eti ni mtu wa kilaji na akishapataga hatakagi shida!
No, Wema anatakiwa kusema sasa basi, hasa baada ya hivi majuzi kuonekana katika picha akiwa na ‘katoto’ kanakodaiwa eti ndiyo ka-mtu kake kwa sasa.
Wema Sepetu akiwa na Idris Sultan.
Kwa nini kila siku Wema? Inawezekana kabisa kuwa ni tabia yake ambayo
siku zote haina dawa, lakini kuna wakati inabidi ujitazame pale ulipo
na kile unachokifanya.Kama kuna mtu anamuongopea kuwa kushiriki na wanaume wengi kutaendelea kulifanya jina lake libakie juu, aachane naye.
Jina linaweza kubakia juu, lakini mwili ukamuangusha.
Unaweza kukarabati sehemu za mwili zikawa kama za mwaka juzi, lakini wakati ukifika, kila kitu kitataka kuwa katika uhalisia wake, jambo ambalo nina uhakika litamfanya ajute sana.
Kwa kifupi nimwambie tu mwanadada huyu kuwa, imekuwa too much, sasa aangalie anawezaje kulirekebisha eneo hili la kubadili wanaume, wakati mwingine anaingia kwa wale ambao katika hali ya kawaida unaona anapita tu.
Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ akizidi kupozi kimahaba na ‘Bob Junior’ kipindi cha nyuma.
Wema ‘This is Too Much’ Bwana!
Reviewed by Erasto Paul
on
November 19, 2016
Rating:
No comments:
Thank you for commenting to Mwanauswahili